Home Habari za michezo KUHUSU KUONDOKA AU KUBAKI YANGA…AZIZI KI AVUNJA UKIMYA….MSIMAMO WAKE MPYA HUU HAPA…

KUHUSU KUONDOKA AU KUBAKI YANGA…AZIZI KI AVUNJA UKIMYA….MSIMAMO WAKE MPYA HUU HAPA…

Habari za Yanga leo

KIUNGO wa Yanga, Stephane Aziz Ki amefungika juu ya hatma yake ya msimu ujao na kuweka wazi kuwa bado hajaongeza mkataba na kuwapa kipaumbele zaidi zaidi mabosi wake hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani.

Aziz Ki ni kinara wa kufamia nyavu kwenye kikosi cha Yanga, ambaye mkataba wake unafikia ukingoni na inadaiwa nyota huyo yupo kwenye mazungumzo na klabu mbili Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs za Afrika kusini lakini Yanga wanapambana  kukihakikisha wanambakiza kiungo huyo.

Aziz Ki amesema kwa sasa bado ni mchezaji wa Yanga licha ya mkataba wake kuwa unafika ukingoni.

Amesema licha ya kupata ofa nyingi kipaumbele chake anawapa Yanga juu ya kuongeza mkataba mwingine kabla ya kufikiria ofa hizo zilizopo mezani kwake.

“Mpaka sasa ni mchezaji wa Yanga, nafasi kubwa zaidi nawapa wao ninamuamini Rais wa Yanga. Hersi (Saidi), ndio aliyenileta hapa, tuna makubaliano yetu kuwa Yanga inapaswa kucheza fainali ya Afrika na tutwae kombe.

Hiyo ndio ndoto yangu na ikitokea tunacheza fainali na kubeba ubingwa nitamfuata Rais Hersi kumuomba baraka zake ili niondoke zangu ila kwa sasa bado malengo yangu na Yanga hayajatimia mpaka tucheze fainali Afrika,” amesema Aziz Ki.

Kuhusu ufungaji bora aliongeza kuwa anachoangalia zaidi ni jinsi ya kuendelea kutafuta pointi tatu na kumaliza ligi kwa heshima ya kutopoteza  kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons

“Sifikirii kuhusu tuzo ya ufungaji bora kwa sasa bali ni malengo ya kupata ushindi kwa timu ipo hivyo, nikipata nafasi nitafunga ama kutoa pasi kwa mchezaji kwani kikubwa nikuona kwamba tunapata matokeo mazuri, “ amesema kiungo huyo.

SOMA NA HII  Infinix NA TIGO WAZINDUA RASMI SIMU KALI YA FUNGA MWAKA.