Home Habari za michezo MCHAMBUZI:- AZIZI KI HAWEZI TENA KUBAKI BONGO….YANGA HAWANA PESA YA KUMPA KWA...

MCHAMBUZI:- AZIZI KI HAWEZI TENA KUBAKI BONGO….YANGA HAWANA PESA YA KUMPA KWA SASA…

Habari za Yanga leo

Wakati Kiungo wa Yanga Raia wa Burkina Faso Stephen Aziz KI akizidi kuonesha makali katka Klabu ya Yanga msimu huu.

Hivi sasa mchezaji huyo anaongoza mbio za ufungaji akimuacha Kiungo wa Azam Feisal Salum mwenye mabao 17, Aziz KI amefikisha mabao 18.

Sasa Mchambuzi wa Michezo kutoka TV 3, Alex Ngereza amesema kwa kiwango alichokionesha mchezaji huyo hapaswi kubaki Yanga msimu ujao.

Akizungumza Alex Ngereza anasema;

“Nitashangaa sana kama Azizi ki ataendelea kubakia Yanga kwasababu Yanga ni timu ndogo Barani africa na haiwezi kumlipa fedha nyingi kama ambazo ataenda kulipwa na vilabu vikubwa barani africa ambavyo vinamhitaji”

AZIZI KI AFUNGUKA HATMA YAKE..

KIUNGO wa Yanga, Stephane Aziz Ki amefungika juu ya hatma yake ya msimu ujao na kuweka wazi kuwa bado hajaongeza mkataba na kuwapa kipaumbele zaidi zaidi mabosi wake hao wa mitaa ya Twiga na Jangwani.

Aziz Ki ni kinara wa kufamia nyavu kwenye kikosi cha Yanga, ambaye mkataba wake unafikia ukingoni na inadaiwa nyota huyo yupo kwenye mazungumzo na klabu mbili Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs za Afrika kusini lakini Yanga wanapambana  kukihakikisha wanambakiza kiungo huyo.

Aziz Ki amesema kwa sasa bado ni mchezaji wa Yanga licha ya mkataba wake kuwa unafika ukingoni.

Amesema licha ya kupata ofa nyingi kipaumbele chake anawapa Yanga juu ya kuongeza mkataba mwingine kabla ya kufikiria ofa hizo zilizopo mezani kwake.

“Mpaka sasa ni mchezaji wa Yanga, nafasi kubwa zaidi nawapa wao ninamuamini Rais wa Yanga. Hersi (Saidi), ndio aliyenileta hapa, tuna makubaliano yetu kuwa Yanga inapaswa kucheza fainali ya Afrika na tutwae kombe.

SOMA NA HII  KUPITIA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET, SLOTI YA STICKY 777 INAWEZA KUKUPA FAIDA KUBWA!