Home news SENZO:HII NDIYO YANGA AMBAYO TUNAITAKA

SENZO:HII NDIYO YANGA AMBAYO TUNAITAKA


 KAIMU Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Yanga 
SC, Senzo Mbatha Mazingisa, amesema kuwa sasa wameanza kuiona Yanga ambayo walikuwa wakitamani kuiona kwa muda mrefu huku akisisitiza kuwa Wanayanga watarajie mambo makubwa msimu huu.

Yanga imefanikiwa kushinda mechi mbili za kwenye ligi ambapo ilianza kushinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera kisha jana ilishinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold.

Akizungumza na Championi Ijumaa, kiongozi huyo alisema kuwa licha ya ushindi walioupata dhidi ya Simba kwenye Ngao ya Jamii na katika ligi, ameweza kuona mabadiliko makubwa kwa Yanga kama timu kwa sababu hata wachezaji wamekuwa wakionyesha kiwango kizuri cha uchezaji tofauti na huko nyuma ambapo Yanga ilikuwa inacheza bila mpangilio.

“Ukitazama jinsi Yanga inavyocheza sasa dhidi ya timu pinzani utaona kabisa timu hii imekuwa na mabadiliko sana tofauti kabisa na michezo ya hapo awali ambapo tulipoteza kimataifa lakini naweza kusema kuwa hii ya sasa ndio Yanga ambayo tulikuwa tukitamani kuiona kama ambavyo inacheza sasa, kuna pasi unaziona zinapigwa wachezaji waonyesha uwezo wao kitimu na uwezo binafsi, ni mabadiliko makubwa kwetu.

“Binafsi naona kabisa tumepiga hatua kubwa,kuanzia tulivyocheza na Rivers United halafu tukacheza na Simba, naona kuna vitu vinaanza kubadilika, hivyo tuna imani kuwa msimu huu kuna mambo mazuri yanakuja kutoka kwa Yanga.

“Tulihitaji muda ili kuwa bora, hivyo tunashukuru ubora tunaanza kuuona, pongezi kwa benchi la ufundi, naona tumeanza na mwanzo mzuri,” alisema Senzo.


SOMA NA HII  HUYU HAPA 'TSHABALALA' AKIWA DUBAI...AIGA MAISHA YA MASTAA WA ULAYA KUPONDA RAHA ....AFUNGUA NJIA KWA WATZ...