Home Habari za michezo BAADA YA KUPEWA MECHI YA KWANZA….GAMONDI ASHINDWA KUJIZUI KUHUSU GUEDE….

BAADA YA KUPEWA MECHI YA KWANZA….GAMONDI ASHINDWA KUJIZUI KUHUSU GUEDE….

Habari za Yanga leo

YANGA inatarajiwa kushuka uwanjani kesho kuivaa Dodoma Jiji katika mechi ya Ligi Kuu Bara, ikiwa ni saa chache tangu ilipotoka suluhu ugenini na Kagera Sugar, mjini Bukoba, huku kocha mkuu, Miguel Gamondi akikunwa na mwanzo mzuri wa Joseph Guede.

Guede aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili, aliingia uwanjani dakika ya 57, kwenye mchezo wa juzi uliopigwa Uwanja wa Kaitaba na kocha Gamondi alisema jamaa ana kitu.

Kocha Gamondi alisema licha yakutostahili sare hiyo ugenini, lakini kwa vile matokeo yameshatokea hawana jinsi, ila kujiandaa kwa mechi zijazo, akieleza wenyeji wao juzi waliamua kucheza mtindo wa kubaki basi na kuwafanya nyota wa Yanga kushindwa kufanya mambo.

β€œNawapa pole mashabiki wa Yanga waliopo Kagera, kwani walikuja kwa wingi kuiona timu lakini hawakuona soka zuri kama walivyotarajia kutokana na aina ya uchezaji wa Kagera. Sisi tulifeli kutengeneza nafasi na kuzitumia, ila tunarudi tukiwa imara kwa mchezo ujao ila wachezaji wanatakiwa kuonyesha njaa zaidi ya kutamani matokeo ya ushindi,” alisema Miguel raia wa Argentina.

Juu ya Guede aliyecheza mechi ya kwanza tangu sajiliwe na Yanga, kocha huyo alisema bado ni mapema mno akitaka apewe muda zaidi, licha ya kukiri ameridhishwa na alivyocheza kwa dakika hizo chache.

β€œNi mchezaji mzuri anayetamani kucheza, hicho ndicho kinachonifurahisha zaidi kwake, japo bado anahitaji muda wa kuzoea timu ila ameonyesha kitu kizuri kwa mwanzoni,” alisema Gamondi.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali, Guende aliingia uwanjani dakika ya 57 sambamba na Kennedy Musonda aliyerejea kutoka Afcon 2023 na alionekana mzuri kwenye mipira ya vichwa, huku akiwa mwepesi wa kuachia mipira kwa mwenzake na kujipanga kwa haraka..

Nyota huyo na wenzake wanarudi Azam Complex kesho kuikabili Dodoma Jiji.

SOMA NA HII  WAKIJIANDAA NA ASEC...PABLO ASHTUKIA 'NCHEZO' CAF..ABADILI GIA ANGANI..KIBWANA AZUA VITA...