Home Habari za michezo VITA YA AZIZ KI NA FEI TOTO YAPAMBA MOTO…KUAMULIWA NA SHERIA HII

VITA YA AZIZ KI NA FEI TOTO YAPAMBA MOTO…KUAMULIWA NA SHERIA HII

FT:- AZAM FC 2-1 YANGA

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephanie Aziz Ki na kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ wanaongoza kwenye mbio za ufungaji bora wakiwa na mabao 15 na assists 7 kila mmoja.

Msimu uliopita kuliibuka mjadala baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele na kiungo wa Simba, Saido Ntibazonkiza kulingana idadi ya mabao kwenye orodha ya uongozi wa ufungaji bora wakimaliza na mabao 17 na mwisho wa siku wote wakapewa tuzo ya ufungaji bora.

Hivi ndivyo mfungaji bora wa ligi kuu 2023-24 atavyopatikana kikanuni:

Kanuni ya 11 (vikombe na tuzo)
13.1. Magoli yaliyofungwa kwa njia ya kawaida yatakuwa na alama mbili (2) na magoli yaliyofungwa kwa njia ya penati yatakuwa na alama moja (1). Mchezaji mwenye alama nyingi atakuwa mshindi.

13.2. Endapo watalingana alama, mchezaji aliyecheza muda mchache zaidi atakuwa mshindi.

13.3. Endapo watafanana katika vigezo vyote viwili hapo juu, mchezaji aliyefunga mabao mengi ugenini atakuwa mshindi.

13.4. Katika mashindano ya mtoano, mshindi atakuwa mchezaji ambaye timu yake imefika hatua ya juu zaidi kuliko mwingine na endapo hatua hii haitatoa mshindi kipengele cha i-iii vitatumika kwa mpangilio wake.
Kwa kanuni hii, nyota wa timu yako atabeba kiatu?

SOMA NA HII  MWAKINYO:- KUNA WATU WANATAKA KUNIKWAMISHA....WANAMPIGIA SIMU MPINZANI...