Home Uncategorized AJIBU ALALA HOTELI YA ROONEY SAUZI

AJIBU ALALA HOTELI YA ROONEY SAUZI


WAKATI Jeshi zima la Simba likiwa linaendelea kujifua kwenye kambi yake nchini Afrika Kusini, imebainika kuwa sehemu hiyo ambayo Simba wameweka makazi paliwahi kukaliwa na timu ya taifa ya England wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.

Simba wamekimbilia Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara sambamba na michuano ya kimataifa ambapo katika msafara wao huo, yupo Ibrahim Ajibu aliyejiunga nao hivi karibuni akitokea Yanga.

Kikosi hicho kinachofundishwa na Mbelgiji Patrick Aussems, kimeweka kambi katika Mji wa Rustenburg, Afrika Kusini ambapo pia mabingwa wa zamani wa nchi hiyo, Orlando Pirates wapo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori ameliambia Championi Ijumaa, kuwa kambi hiyo ni bora kwani iliwahi kukaliwa na timu ya taifa ya England wakati walipokuwa wakishiriki Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

“Watu wasione kwamba tumeweka kambi kule Afrika Kusini wakadhani kwamba ni kambi tu ya kawaida. “Mahali ambapo sisi tumeweka kambi, England waliwahi kukaa pale wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.

“Hilo eneo ni zuri na lina vifaa vyote ambavyo mwalimu amevitaka kwa ajili ya kujenga stamina kwa timu pamoja na mazoezi mengine,” alisema Magori. Miongoni mwa nyota wa England ambao walikaa katika kambi hiyo waliopo Simba kwa sasa ni Wayne Rooney, John Terry, Steven Gerrard, Frank Lampard na Peter Crouch.

SOMA NA HII  TAZAMA MAKALI YA KIPYA MPYA ANAYETAJWA KUTUA YANGA - VIDEO