Home Uncategorized BIGIRIMANA AANZA KUITISHA SIMBA

BIGIRIMANA AANZA KUITISHA SIMBA


KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amesema kuwa katika kuthibitisha ubora wa ufungaji anaanza na AS Vita wanafuatia watani wao Simba.

Staa huyo aliitoa kauli hiyo, akiwa kambini mkoani Morogoro ambako wameingia tangu Jumatatu iliyopita wakijiandaa na msimu mpya wa ligi pamoja na tamasha lao la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika Agosti 4, mwaka huu.

Katika tamasha hilo, Yanga wanatarajiwa kucheza mchezo mmoja wa kirafi ki wa kimataifa dhidi ya AS Vita utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bigirimana alisema kuwa anafahamu uwezo wake, hivyo kwa kuanza atauonyesha kwenye mchezo huo wa kirafi ki dhidi ya AS Vita.

Bigirimana alisema, anafahamu AS Vita wapo baadhi ya wachezaji wanaomfahamu, lakini hilo halimpi shida na badala yake atahakikisha anaonyesha makali yake baada ya kutoka kambini huko Morogoro.

“Ninafahamu Mashabiki wa Yanga wana imani na mimi na kikubwa ninataka kuwathibitishia ubora wangu kwa kuanzia mchezo huu wa kirafi ki dhidi ya AS Vita.

“Baada ya mchezo huo watafuata wapinzani wetu Simba, mchezo ninaousubiria kwa hamu kubwa mara tutakapokutana nao.

“Mimi hizo derby ndiyo ninazozipenda, kikubwa ninataka kuwaonyesha uwezo wangu, katika kila mchezo ninataka kufunga bao ili nitengeneze historia kubwa ndani ya Yanga,” alisema Bigirimana.

SOMA NA HII  TAREHE YA JEMBE JIPYA KUTUA SIMBA YATAJWA,NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA