Home Simba SC BARBARA AWAPIGIA “SALUTI” AL AHLY

BARBARA AWAPIGIA “SALUTI” AL AHLY


LICHA ya Simba kuongoza kundi lao katika michuano ya klabu bingwa, viongozi wa wekundu hao wamewakubali wapinzani wao Al Ahly kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya ndani ya timu yao.

Simba inatarajia kumaliza mchezo wao wa mwisho leo saa 4:00 usiku Nchini Misri mchezo ambao haina cha kupoteza baada ya kukata tiketi tayari ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez, amekubali mziki wa Al Ahly kwa namna ambavyo wameendelea kitendo kinachowafanya kuzidi kuwa na alama kubwa katika ukanda wa Afrika.

Katika ukurasa wake wa Instagram Barbara ameandika “Kiuhalisia timu ya Al Ahly inabaki kuwa alama kwa timu za mpira wa miguu barani Afrika, hii inakwenda mbali zaidi hadi nje ya uwanja kutokana na hayo tunapaswa kuhamasika na vitu kama,”

“Uwekezaji na Miundombinu, kiuchumi na miundo na mifumo ya utendaji na uendeshaji, tathimini ya wachezaji na mali nyingine, uchambuzi wa mitandao ya kijamii na utendaji wa kimichezo,”ameandika Barbara katika ukurasa wake.

Simba katika michezo yake mitano imemfunga Al Ahly bao 1-0, As Vita bao 1-0, El Merrikh 0-0, El Merrikh bao 3-0 pamoja na As Vita mabao 4-1 ikiongoza kundi hilo kwa jumla ya pointi 13 huku Al Ahly akiwa na pointi nane ambao wote wamesonga mbele hatua inayofuata.

SOMA NA HII  NAMNA SIMBA WALIVYOPAMBANIA POINTI TATU DODOMA