Home Habari za Usajili DIRISHA LA USAJILI LAFUNGULIWA…SIMBA, YANGA ZAANZA NA MAJINA HAYA

DIRISHA LA USAJILI LAFUNGULIWA…SIMBA, YANGA ZAANZA NA MAJINA HAYA

HABARI ZA USAJILI

Dirisha la Usajili (FIFA Connect) kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC (NBCPL), Championship League (CL), First League (FL) na Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) msimu wa 2024/2025 limefunguliwa leo Jumamosi Juni 15, 2024 na litafungwa Agosti 15 2025.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limezitaka vilabu kufanya usajili na uhamisho wa wachezaji huku ikisisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Aidha usajili na uhamisho wa wachezaji kwa dirisha dogo utafunguliwa Desemba 16, 2024 na kufungwa Januari 15, 2025.

Tayari vilabu vingi haswa vya Ligi kuu vimeanza kujipanga kufanya usajili na kwa baadhi ya wachezaji wamekwisha sajili, bado kutambulishwa tu.

Klabu ya Simba ni moja kati ya timu inayotupiwa jicho sana kwenye usajili msimu huu, na wao kupitia Uongozi wao walinukuliwa wakisema msimmu huu wamejipanga na tayari mchakato wa kusajili nyota kadhaa wa kimataifa umeanza.

Kwa upande wa Yanga tetesi za usajili hazisikiki sana kwa sababu klabu hiyo, imekuwa na wachezaji wengi wazuri hivyo hata wakiingia sokoni, watahitaji kufanya kufanya sajili chache ili kuongeza nguvu kwenye timu yao.

Upande wa Rais wa Yanga Injinia Hersi alisema kwamba msimu huu wamejipanga kufanya sajili zenye tija na zitakazoongeza nguvu.

Azam FC tayari wamshatambulisha nyota kadhaa kwenye kikosi chao, na wao watakipiga Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, hivyo wameanza kufanya maandalizi mapema, ili kujipa muda mzuri wa pre season.

SOMA NA HII  SILAHA YA AZIZ KI NI HAPA...KILA KITU KITAJULIKANA