Home Habari za Simba Leo SIMBA KUSHUSHA CHUMA…ANATOKA CONGO…NI MWAMBA HASWA

SIMBA KUSHUSHA CHUMA…ANATOKA CONGO…NI MWAMBA HASWA

Habari za Simba

Klabu ya Simba inatajwa kukamilisha usajili wa kiungo kutoka Jamhuri ya Congo Debora Mavambo Fernandes (mwenye jezi nyeupe pichani juu) aliyekuwa aakiitumikia Mutondo Stars ya Ligi Kuu Zambia (MTN).

Kiungo huyo wa kati mzaliwa wa Angola mwenye umri wa miaka 24 tayari yuko nchini na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakaotambulishwa na Simba siku chache zijazo.

Debora ameitumikia Mutondo FC msimu mmoja akijiunga akitokea klabu ya Academica Petroleos do Lobito ya Angola mwaka 2023.

Kiungo huyo anamudu kucheza eneo la kiungo mkabaji lakini pia mara chache ametumika katika safu ya ulinzi.

Ujio wa Debora huenda ukashuhudia Simba ikiachana na Sadio Kanoute au Babacar Sarr.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema uongozi uko kwenye majadiliano ya kusitisha mikataba ya baadhi ya wachezaji.

Wachezaji wa Simba wanatakiwa kuanza kuripoti Dar kuanzia Julai 1, ili kufanya mazungumzo kabla ya timu hiyo kwenda kuanza maandalizi ya msimu huko Misri.

Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally akizungumzia usajili wa timu hiyo amesema kwamba, usajili wao umekamilika kwa asilimia 97%.

“Usajili wetu umekamilika kwa 97%, hivyo muda wowote tunaanza kutambulisha vyuma vipya, kuna huyo mchezaji tumemsajili ni mrefu zaidi ya goli, haruki anafunga tu”

“Kuna mchezaji mwingine anatoka DR Congo, na kuna huyo mmoja anakimbia kama treni mpya SGR” Alisema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  SIMBA SC HATUJAMALIZA ZOEZI LA USAJILI, VYUMA VINGINE HIVI HAPA