Home Habari za Yanga Leo ENG HERSI HAPOI…USAJILI WA MSIMU HUU…NI KUFURU

ENG HERSI HAPOI…USAJILI WA MSIMU HUU…NI KUFURU

Habari za Yanga

RAIS wa Yanga na Mwenyekiti wa Vilabu vyote barani Afrika Eng Hersi Said, hataki kupoa hata kidogo, ni baada ya kutoboa siri ya klabu hiyo kuhusu sajili za maana kwa msimu ujao wa 2024/25.

Eng Hersi alisema kwamba licha ya timu yake kutesa sana msimu uliomalizika na usiku wa kuamkia Juni 3, kutwaa ubingwa wa 8 wa Kombe la Shirikisho na wa 4 mfululizo tangu michuano hiyo irejee tena kwa mara nyingine mwaka 2015/16 kutokanaa na kusimama kwa kipindi kirefu zaidi kuanzia mwaka 2003.

Akizungumza baada ya mchezo huo wa fainali kumalizika, Eng Hersi akiwa ni mwenye furaha sana kwa mafanikio ya timu alijikuta akitoboa mambo ya usajili ambao ameutaja kuwa utakwenda kuboresha kikosi hicho cha Wananchi.

“Haikuwa rahisi, mchezo ulikuwa mzuri na hadhi ya fainali, nimpongeze Gamondi, lakini mwaka huu hatukuwa bora sana kwenye mikwaju ya Penati, tulipoteza dhidi ya Simba, na Mamelodi na leo na Azam FC, mashabiki na wanachama wameona ila niwapongeze wachezaji na benchi la ufundi kwa ubingwa huu”

“Tunaendelea kujenga timu imara, na kusafanya sajili nzuri kuendelea kuimarisha timu yetu ili iwe na ushindani mkubwa zaidi” Rais wa Yanga- Eng Hersi Saidi

Utakumbukwa hivi karibuni, Hersi alisafiri kwenda DR Congo katika klabu ya TP Mazembe, ikielezwa kuwa kuna fundi wa mpira alienda kukamilisha usajili wake.

Klabu ya Yanga kwa msimu uliomalizika umekuwa na mafanikio makubwa, wametwaa taji la Ligi Kuu Bara kwa mara 3 mfululizo na likiwa taji lao la 30.

Juni 02, utabaki kuwa kwenye historia ya wachezaji hao kwamba ni siku ya furaha kwao, lakini kwa upande wa Azam FC utabaki kuwa na machungu zaidi kwa kupoteza taji lao la pili la FA, kwa mikwaju ya penati 5-6.

SOMA NA HII  MMH KUMBE ISHU YA FEI TOTO...NI KAMA YA MSUVA ILIVYOKUWA...YANGA KUWENI MAKINI