Home Habari za Usajili Yanga SAKATA LA LOMALISA LAMUIBUA MWINYI ZAHERA…HATMA YAKE YANGA

SAKATA LA LOMALISA LAMUIBUA MWINYI ZAHERA…HATMA YAKE YANGA

Habari za usajiri Yanga

BAADA ya kuitumikia Yanga kwa misimu miwili, beki Mkongomani, Joyce Lomalisa anatajwa kutua Namungo FC kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Lomalisa awali alikuwa anatajwa kujiunga Simba lakini mambo yakaenda tofauti na sasa inaelezwa Namungo inayonolewa na Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera ina mpango wa kumpa mkataba wa miaka miwili staa huyo mwenye mataji mawili ya Ligi Kuu Bara.

Beki huyo mwenye uwezo wa kuanzisha mashambulizi na kupiga krosi zinazofika katika maeneo sahihi, pia ameshinda mataji mawili ya Kombe la Shirikisho (FA) akiwa na Yanga na kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023.

Zahera anataka kuijenga Namungo kuwa tishio msimu ujao na anasaka wachezaji wenye uzoefu na mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara watakaoifanya timu hiyo kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo.

Kinachoendelea kwa sasa Simba baada ya Mohammed Dewji ‘Mo’ kukataa usajili wa beki huyo, sasa ni rasmi atajiunga na Miamba hiyo ya kusini mwa Tanzania.

Simba kwa sasa wameingia sokoni kutafuta beki mwingine wa kushoto atakayempa changamoto Mohammed Hussein ambaye amedumu Simba kwa misimu 10.

Tangu ajiunge na Simba mwaka 2014, amekuwa na kiwango kizuri kiai cha kuwa na uhakika wa namba kwa kila kocha anayekuja pale.

Je Simba watapata mbadala wa Mohamed Hussein kwenye eneo la beki wa kushoto.

SOMA NA HII  RASMI....MANARA AMATAMBULISHA MORRISON YANGA...ATUMIA NJIA YA 'KININJA' KWA KUMTAJA KUWA MCHEZAJI BORA....