Home Habari za Simba Leo FARHAN: MSIPENDE MCHEZAJI…IPENDENI SIMBA…ZAMA ZA CHAMA ZIMEPITA

FARHAN: MSIPENDE MCHEZAJI…IPENDENI SIMBA…ZAMA ZA CHAMA ZIMEPITA

HABARI ZA SIMBA

Mchambuzi wa Michezo na Shabiki wa Simba Farhan Kihamu amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo, kuipennda zaidi timu kuliko mtu, mchezaji au mtendaji kwani ni watu wanaaokuja na kupita, ila timu itaendelea kuwepo.

Farhan Aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba “SHABIKI WA SIMBA nisikilize tu kidogo, mpira wa miguu ni burudani lakini kwa upande mwingine ni biashara, anayeipenda klabu ni SHABIKI na anayefanya kazi ya mpira ni MCHEZAJI, mmoja anaburudika na mmoja kati ya hao wawili yupo kibaruani, hata wewe ambaye ni Shabiki una ajira yako pengine sehemu huwa unahama kufuata maslahi mazuri, ndio kama ilivyo kwenye soka.”

“CHAMA tayari ameondoka klabuni, ni sehemu ya football ila SIMBA imesalia na itaendelea kuwepo, hata kama asingeondoka basi kuna siku angestaafu na maisha yangeendelea, ni sahihi kuumia ila ni sahihi zaidi kutopanic na kutupiana lawama yoyote kwa Viongozi au Mchezaji kwakuwa hii ni biashara kuna kukubaliana na kutokubaliana.”

“SHABIKI wewe ipende hii logo pichani, fahamu ni wewe pekee hutohama ila wengine woote wanakuja na kuondoka haswa Wafanyakazi wakiwemo Wachezaji, Messi Lionel ameondoka Barcelona, pale Liverpool walimtengeneza Michael Owen ila akasepa zake, Chelsea tulimpika Hazard akasepa zake, Man United walimtengeneza Beckham ila akaondoka, ni kawaida sana kwenye dunia ya mpira.”

“SIMBA aliwahi kuondoka Juma Kaseja kwenye ubora wake, Emmanuel Okwi kwenye ubora na wengine wengi tu ila klabu iliendelea na wachezaji wengine akiwemo CHAMA ambaye alijenga Ufalme wake, leo umetamatika hivyo klabu itapaswa kuanza maisha mpya na zama mpya, tukubaliane kwa pamoja kuwa nothing is there forever.”

“Sisi kama klabu tuna mengi ya kufanya haswa wakati huu focus yetu ni kupaza sauti kuwahimiza wasajili Wachezaji wa maana, tushauri, tukae chini kama klabu ili tufike sehemu kubwa na nzuri, huu sio wakati wa kunyoosheana vidole wala kupishana bali kuanza mwanzo mpya ambao sote tunautaka, anayehisi hajapenda ahame tu klabu, wala sio suala ila football ni kawaida sana hivi vitu.”

“Tukae nyuma ya timu, tusupport Wachezaji wote ambao watasajiliwa na tukubali kuwa TRIPLE C ameshaondoka, ila timu haiwezi kufa, maisha yataendelea na tumtakie heri kwenye changamoto mpya.”

SOMA NA HII  SIMBA HALI SI SHWARI LIGI KUU...... NAMUNGO WAFANYA UKATILI WA KULAZIMISHANA