NI MWEZI wa Usajili na Vimbwanga vyake, Tumesikia habari za Chama na Yanga na sasa tuna hii ya Prince Dube baada ya kumalizana na Azam FC na kuhusishwa zaidi na Yanga, kuna mapya yameibuka kumhusu Mshambuliaji huyo wa Zimbabwe.
Sakata la muda mrefu la Prince Dube lilikamilika baada ya mchezaji huyo raia wa Zinbabwe kutii amri na kulipa ‘pesa za watu’ kama walivyokubaliana kwenye mkataba.
Lakini wiki hiyo hiyo Azam FC tena walimpoteza winga wao hatari kutoka Ivory Coast, Kipre Jr. aliyeuzwa kuelekea MC Alger ya Algeria.
Katika biashara hizi mbili Azam FC wameingiza zaidi ya Sh 1 Bilioni za kitanzania, kwa hiyo unaweza kusema wamefanikiwa kiuchumi.
Lakini wakati huo huo wamepoteza wachezaji wao muhimu sana kikosini, hiyo ni hasara kiufundi.
Sote tunajua kilichotokea kwa Dube, lakini hatujui vizuri kuhusu Kipre Jr. Mtu anaweza akadhani mchezaji huyo aliyemaliza msimu wa 2023/24 akiwa na mabao 9 na pasi 9 za mabao, ameuzwa kama biashara ya kawaida ya wachezaji, hapana.