KLABU ya Simba SC imepanga kumtoa kwa mkopo au kumuacha moja kwa moja winga wao wa Kimataifa wa Ivory Coast Aubin Kramo.
Uongozi wa Simba unaelezwa kuwa umetaka kumpunguzia mshahara kwa asilimia kubwa kama anataka kuendelea kusalia ndani ya kikosi hicho jambo ambalo amegoma kuliafiki.
Hivyo Uongozi wa juu ukaafiki wamtoe kwa mkopo wa miezi 6 kwenda Timu nyingine kisha baadaye atarejea ndani ya Klabu jambo ambalo pia ameshindwa kuliafiki na kutaka aondoke moja kwa moja kwakuwa mkataba wake umebakia mwaka mmoja tu na sio kutolewa kwa mkopo.
Uongozi wa Simba tayari umemtafutia Timu ya kwenda kujiunga nayo kama ataafiki kutolewa kwa mkopo atatua Al Ahli ya Libya kwa mkopo wa miezi 6 au kwa mkataba wa moja kwa moja.
Mchezaji mwenyewe anasema yupo fiti asilimia mia moja na amerejea rasmi dimbani mara baada ya kutoka kwenye majeraha ya muda mrefu aliyokuwa akijiuguza,
Aubin Kramo anaona yupo fiti na ana uwezo wa kucheza na kugombania nafasi na wachezaji waliopo ndani ya Simba, swala la yeye kutolewa kwa mkopo hajaliafiki hivyo basi anaona ni bora aondoke moja kwa moja kama ni timu atatafuta yeye mwenyewe.
Aubin Kramo wiki hii atarejea Tanzania kuchukua vitu vyake na kisha kurejea nchini kwao Ivory Coast kwenda kujipanga upya, kujua mustakabari wake baadae utakuwaje.