Home Habari za Yanga Leo SABABU ZA KUCHELEWA UTAMBULISH WA BEKI WA YANGA..CHADRACK BOKA

SABABU ZA KUCHELEWA UTAMBULISH WA BEKI WA YANGA..CHADRACK BOKA

CHADRACK BOKA

BEKI WA KUSHOTO fundi kabisa Chadrack Boka (24) ndiye mchezaji wa 1 kusajiliwa na Yanga SC 2024|25.

Chadrack Boka amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga na kinachosubiriwa ni (ITC) yake pekee.

UTATA UMEANZIA HAPA

Inasemekana amechelewa kuwasili nchini Tanzania kwa sababu klabu aliyotoka FC Lupopo haikutaka mchezaji huyo aondoke. Hivyo walikuwa wanaweka ngumu sna kumshawishi abaki ili kuitumikia klabu hiyo.

FC Lupopo wanadai mchezaji huyo ni wao wamekiambia Chama cha soka Nchini DRC (FA) kisitume (ITC) kwenda Yanga SC kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

Mchezaji na menejimenti yake wanapambana kutafuta (ITC) ili awahi kuripoti kambini nchini Tanzania kuanzia July (8).

Mchezaji huyo aliyefanya vizuri katika ligi kuu ya DR Congo sio mchezaji wa FC Lupopo, ni mchezaji wa Real Of Kinshasa alijiunga na FC Saint Eloi Lupopo kwa mkopo.

Yanga SC walishamalizana na klabu yake, FC Lupopo ndio waliochelewesha (ITC) yake.

Ieleweke kwamba Tayari klabu ya Yanga imeshaachana na beki wake wa kushot Joyce Lomalisa, na Boka ndiye mrithi wa Lomalisa.

Klabu ya Yanga hadi sasa imetangaza usajili mmoja tu wa KIUNGO Clatous Chama ambaye mkataba wake na aajiri  wake wa zamani Simba SC ulimalizika tangu June 30   mwaka 2024, na hawakutaka kumuongeza mkataba mpya.

Wanachokifanya Yanga kwa sasa ni kuwabakiza wachezaji wao tegemezi, na hadi sasa wamewaongeza mikataba wacheza kama Diarra, Mwamnyeto, Fardi Mussa, na Nickson Kibabage.

SOMA NA HII  YANGA SC YAIBUKA NA HILI...YAMFUA MORISSON SPESHO KWA AJILI YA SIMBA