Home Habari za Simba Leo SIMBA KAMA MASANDAWANA TU…BENCHI ZIMA WANATOKA AFRIKA KUSINI

SIMBA KAMA MASANDAWANA TU…BENCHI ZIMA WANATOKA AFRIKA KUSINI

Habari za Simba, Fadlu Davids

Kocha Fadlu Davids ametangazwa kuwa kocha mkuu wa Simba SC, baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 43 amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi cha Simba SC.

Kabla ya kujiunga na Simba SC, Fadlu alikuwa kocha Msaidizi wa mabingwa wa soka nchini Morocco Raja Club Athletic maarufu Raja Casablanca

Fadlu ambaye enzi zake alikuwa akicheza katika nafasi ya ushambuliaji anachukua nafasi ya Abdelhak Benchikha ambaye aliondoka wakati msimu wa 2023/24 ukiwa unaelekea ukingoni.

Mara nyingi Fadlu amekuwa muumini wa mfumo wa 4-2-3-1 ambao amekuwa akiutumia katika kila timu anayofundisha.

Ameondoka na majembe mawili ya muhimu zaidi yaliyokuwa kwenye benchi la ufundi la Raja, Darian Wilken atakuwa msadizi wake na Mueez Kajee mtathimini mchezo pale Msimbazi kama alivyokuwa Raja.

Aidha, amemchukua Riedoh Berdien kama kocha wa viungo ambaye msimu uliopita alikuwa timu ya taifa ya Ufilipino lakini kabla ya hapo amewahi kufanya kazi Yanga msimu wa 2019/2020 chini ya Luc Eymael aliyefukuzwa na baadaye akafuata Zlatko Krimpotic lakini pia amewahi kuwa kwenye benchi la timu za taifa za Togo, Gambia, Bangladesh na Botswana.

Pia Uongozi wa Simba umeachana na aliyekuwa kocha wao wa Magolikipa Dani Cadena na hivyo Fadlu Davids amekuja na kocha mpya wa makipa, anaitwa Wayne Sandilands.

Benchi zima la ufundi la Simba limeundwa na watu kutoka Afrika Kusini, Simba wanaamini kwenye uwezo na ubora wa makocha kutoka nchi hiyo.

Moja ya vigogo wa Simba jina linahifadhiwa ametaja sababu kuu ya kumchagua Fadlu Davids ni kutaka kutengeneza timu mpya ambayo kila mmoja atakuwa na kiu kubwa ya mafanikio.

“Tunaanza upya. Tunasuka timu ya kisasa ambayo kila mmoja atakuwa na kiu ya kufanya vizuri. Ukiangalia kuanzia kwa wachezaji tunaowasajili, ni vijana wadogo wenye malengo makubwa hivyo hivyo kwa benchi la ufundi,” alisema kigogo huyo na kuongeza;

SOMA NA HII  FADLU DAVIDS ANATAKA SIMBA YA MABAO MENGI...AANZA NA VIUNGO NA WASHAMBULIAJI