Home Habari za Simba Leo RAJA CASABLANCA IPO SIMBA..FADLU DAVIDS KOCHA MPYA ANAYETAMBA NA MIFUMO HII

RAJA CASABLANCA IPO SIMBA..FADLU DAVIDS KOCHA MPYA ANAYETAMBA NA MIFUMO HII

habari za imba, Fadlu Davids

Ni kama Raja imehamia Msimbazi kwani ukiachana na kocha mkuu wa wakali hao wa Morocco, Inaelezwa kwamba Fadlu Davids anayepewa nafasi kubwa zaidi kujiunga na Simba.

Ameondoka na majembe mawili ya muhimu zaidi yaliyokuwa kwenye benchi la ufundi la Raja, Darian na Kajee ambao mmoja atakuwa msaidizi wake na mwingine mtathimini mchezo pale Msimbazi kama alivyokuwa Raja.

Aidha, amemchukua Riedoh Berdien kama kocha wa viungo ambaye msimu uliopita alikuwa timu ya taifa ya Ufilipino lakini kabla ya hapo amewahi kufanya kazi Yanga msimu wa 2019/2020 chini ya Luc Eymael aliyefukuzwa na baadaye aka-fuata Zlatko Krimpotic lakini pia amewahi kuwa kwenye benchi la timu za taifa za Togo, Gambia, Bangladesh na Botswana.

Moja ya vigogo wa Simba jina linahifadhiwa ametaja sababu kuu ya kumchagua Fadlu Davids ni kutaka kutengeneza timu mpya ambayo kila mmoja atakuwa na kiu kubwa ya mafanikio.

“Tunaanza upya. Tunasuka timu ya kisasa ambayo kila mmoja atakuwa na kiu ya kufanya vizuri. Ukiangalia kuanzia kwa wachezaji tunaowasajili, ni vijana wadogo wenye malengo makubwa hivyo hivyo kwa benchi la ufundi,” alisema kigogo huyo na kuongeza;

“Fadlu ni kocha ambaye pia amewahi kucheza soka, ana kiu ya kufanya vizuri lakini pia anatufaa kwenye falsafa yetu kwani ni kijana na sisi tunataka soka la kisasa ndio maana hata wasaidizi wake tumemwambia atafute yeye ili awe na uhuru mkubwa katika kufanya kazi.”

KAZI IPO HAPA

Fadlu na wasaidizi ndani ya Simba wataenda kukutana na kazi kubwa ya kujenga timu mpya baada ya chama hilo kua-chana na rundo la wachezaji waliokuwapo na kushusha wapya. Hapo watatakiwa kujenga timu huku wakiendana na kasi ya mashindano ambayo Simba itashiriki kwa msimu ujao.

Jambo jingine ambalo Fadlu Davids na wasaidizi wake watakutana nalo kikosini hapo ni presha. Hii ni presha ya matokeo chanya ambayo ipo Simba kwa sasa.

Kila mtu ndani na nje ya timu hiyo anataka kufanya vizuri na kupata matokeo mazuri ukizingatia timu hiyo imeyumba kwa misimu mitatu iliyopita. Fadlu Davids atatakiwa kutuliza presha hii na kuhakikisha timu inatulia na kufanya vizuri uwanjani.

SOMA NA HII  RAISI WA SIMBA MO DEWJI AFANYA KUFURU HASWAAA...MECHI YA TAIFA STARS VS UGANDA