TAA ZASIMAMISHA MECHI ZAIDI YA DK 16...TANZANIA VS UGANDA...ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI
Habari za michezo

TAA ZASIMAMISHA MECHI ZAIDI YA DK 16…TANZANIA VS UGANDA…ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI

Marce Ben Komba March 29, 2023 9:12 am

Mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Uganda umesimama kwa muda kufuatia taa za uwanjani kupungua mwanga wakati mchezo ukiendelea.

Dakika ya 37 mwamuzi wa mchezo Ibrahim Traore alisimamisha mchezo huo kufuatia hitilafu hiyo huku akiwapa nafasi wachezaji kupata mapumziko mafupi ya kupata maji.

Hata hivyo baada ya wachezaji kumaliza dakika Moja ya kupata maji bado taa hizo zilikuwa hazijarudi katika ufanisi wake zikiwaka chache tofauti na wakati mchezo ulipoanza.

Hali hiyo imeleta sintofahamu kwa mashabiki wanaofuatilia mchezo huo huku maafisa wa mchezo huo wakiwemo waamuzi na mechi kamishna wakijadiliana kusubiri muafaka wa kurejea kwa mwanga zaidi.

Zaidi ya dakika 16 zikitumika kusubiri taa hizo kuongezeka Mwanga

TANZANIA 0-1 UGANDA TAIFA STARS WALA KICHAPO…NDOTO ZA AFCON BYE BYE…MICHO AONYESHA UBABE BEKI WA SIMBA SHOMARI KAPOMBE “MECHI NA RAJA CASABLANCA…NI MAZOEZI TU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply