BEKI WA SIMBA SHOMARI KAPOMBE "MECHI NA RAJA CASABLANCA...NI MAZOEZI TU
Habari za michezo

BEKI WA SIMBA SHOMARI KAPOMBE “MECHI NA RAJA CASABLANCA…NI MAZOEZI TU

Marce Ben Komba March 29, 2023 9:23 am

BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amesema mchezo wa
marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Aprili 1, 2023 nchini Morocco utakuwa na faida mara mbili.

Mlinzi huyo wa kulia, Kapombe amedai kwakuwa tayari
wameshafuzu hatua ya Robo Fainali hivyo watautumia mchezo huo na Raja CA kama sehemu ya maandalizi kuelekea hatua inayofuata.

“Mchezo utakuwa mgumu, Raja ni timu kubwa Afrika na tunaenda kwao. Tayari tumefanikiwa kutinga robo fainali hivyo tutautumia mchezo dhidi ya Raja kama sehemu ya maandalizi sababu ni mechi ya mwisho ya kundi,” amesema Kapombe.

TAA ZASIMAMISHA MECHI ZAIDI YA DK 16…TANZANIA VS UGANDA…ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI PAMOJA NA BALEKE KUANZA KUTUPIA SIMBA…MBRAZILI KAMTAZAMA WEE..KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HAYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply