Home Habari za Yanga Leo KAMBI YA YANGA IMENOGA…AUCHO NA DIARRA WAONGEZA MZUKA

KAMBI YA YANGA IMENOGA…AUCHO NA DIARRA WAONGEZA MZUKA

Habari za Yanga-DIARA

Nyota wa Yanga SC, Khalid Aucho, Kennedy Musonda na Djigui Diarra, wamerejea nchini na moja kwa moja wameingia kambini kuungana na wenzao kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa 2024-2025.

Khaleed Aucho raia wa Uganda, Musonda na Diarra kutoka Mali, wamechelewa kuingia kambini baada ya kuwa na ruhusa maalum ya mapumziko ambayo sasa imemalizika.

Kurejea kwa wachezaji hao kunafanya kikosi hicho hivi sasa kuwa kamili katika maandalizi kuelekea msimu ujao baada ya kambi kuanza wiki iliyopita Julai 8, 2024.

Ikumbukwe kwamba, siku tatu za kwanza za maandalizi, kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi Gymkhana na Ufukwe wa Coco, kisha Alhamisi kikahamia Avic Town kuweka kambi na kufanya mazoezi ya uwanjani.

Jana Jumapili ilikuwa ni siku ya mapumziko ambapo leo Jumatatu ratiba inaendelea, asubuhi mazoezi yakifanyika Gymkhana na jioni itakuwa zamu ya Avic Town.

Ali Kamwe, Afisa Habari wa Yanga akizungumzia usajili mpya wa Yanga kwa msimu huu alisema kwamba haikuwa kazi rahisi kuwapata wachezaji wenye uwezo mkubwa hilo lipo wazi na linaongeza thamani ya ligi ya Tanzania.

“Msimu huu hata msiposema mawe yatazungumza kwamba Yanga tuna timu bora kwa kuwa kuna wachezaji wazuri wenye ubora na hilo linafanyika kwa sasa kuwa imara kila eneo ndani ya uwanja.

“Kila Mwanayanga anafurahi kwa sasa kwa sababu kila eneo kuna wachezaji bora na wenye uwezo mkubwa hili linatupa nguvu ya kuwa imara kwenye mashindano ambayo tutashiriki.”.

Usajili wa kwanza ndani ya Yanga ambao umeleta mtikisiko Bongo ni wa Clatous Chama ambaye ameibuka hapo bure akitokea Simba yeye ni kiungo mshambuliaji.

Saini ya Stephene Aziz Ki ambaye alitambulishwa Julai 10 kuwa bado ni Mwananchi ilizua gumzo barani Afrika kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za timu mbalimbali.

Hadi sasa Yanga imewatambulisha wachezaji kadhaa akiwem Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka na Abubakar Khommeiny ambaye ni mlinda mlango, na Aziz Andabwile na Duke Abuya.

SOMA NA HII  KWA MOTO WA SIMBA… AZAM WAJITAFUTE SANA