Home Habari za Simba Leo AHMED ALLY ATEMA CHECHE USAJILI WA AHOUA…KUHUSU HATMA YA JOBE AWEKA WAZI.

AHMED ALLY ATEMA CHECHE USAJILI WA AHOUA…KUHUSU HATMA YA JOBE AWEKA WAZI.

Habari za Simba, Ahmed Ally na Ahoua

AFISA HABARI wa Simba Ahmed Ally amesema kwamba usajili wa MVP wa Ivory Coast ulikuwa na vita kubwa sana, lakini pia ameweka wazi juu ya hatma ya mshambuliaji wao Par Omar Jobe ambaye mashabiki wengi wanataka aondoke klabuni hapo.

Ahmed Ally alisema kwamba mchezaji huyo alistahili kwenda kucheza Ulaya lakini akaichagua Simba ambayo ilimpatia ofa nzuri sana, huku yeye mwenyewe akiwa na dhamira ya kukua na kufanya makubwa.

“Msimu uliopita safu yetu ya ulinzi iliruhusu mabao mengi sana, haikuwa na uwiano sawa tukamuuza Henock Inonga na Kennedy Juma, tumewasajili Lameck Lawi na Hamza”

“Kwa Tanzania akiwa mzuri anafikiria Simba na Yanga, lakini kwa mchezaji wa Ivory Coast akiwa mzuri huwaza kwenda Ulaya, lakini Ahoua tulimpa pesa kubwa ambayo ilimbadilisha mawazo ya kwenda Ulaya na kuichagua Simba”

“Ahoua hauna kitu cha kumwambia, mtaani kwao anawaona kina Drogba walivyofanikiwa, na yeye anaona fursa kwenye mpira ili afanikiwe”

“Ni nafasi nzuri kwa Ahoua akiitumia sawaswa atanufaika kwa nfasi aliyopata” Amesema Ahmed Ally.

Ahmed Ally aliendelea kuelezea idadi ya washambuliaji ambao timu hiyo itaondoka nao kwenda kufanya maandalizi ya msimu ujao 2024/25, huku akitaja hatma ya Par Omar Jobe.

“Washambuliaji wa Simba ambao tutaenda nao wiki ijayo Pre Season Misri ni wawili, Steve Mukwala ambaye leo amefanya vipimo na Fredy Michael, huyo mwingine sina taarifa zake kutoka kwa Viongozi”

“Niwatoe wasiwasi mashabiki wa Simba washambuliaji tegemeo kwa sasa wa Simba SC ni wawili na kuna mwingine mzawa anakuja” Ahmed Ally.

Pia Ahmed Ally aliweka wazi baadhi ya maeneo maeneo ambayo Simba wanaenda kuimarisha, katika usajili huu wa dirisha kubwa.

“Bado beki wa kati anakuja, upande wa kushoto kuna mchezaji mmoja anakuja kumpa changamoto Muhammed Hussein ambaye anacheza mechi nyingi, ikiwemo kumpumzisha Tshabalala ili kulinda ubora wake hata kwa mismu minne, kuliko kulazimisha kucheza yeye tu kila siku”

“Hapa ieleweke sawa, anakuja kusaidiana na Tshabalala sio kushindana, eneo la kiungo mkabaji tunashusha chuma, na kuna wengine viungo wachezeshaji kwajili ya kuja kumaliza usajili, kwa ujumla ni kama mashine 6 zimesalia kukamilisha usajili wetu” Ahmed Ally’

SOMA NA HII  TIMU YA MSUVA KUSHUKA DARAJA...ACHEZA LIGI MOJA NA RONALDO...AMEZUNGUMZA HAYA