Home Habari za michezo BHAASIIII….BALEKE NAYE HUYOOOO JANGWANI…..DILI ZIMA LIMEMALIZWA SALAMANDA….

BHAASIIII….BALEKE NAYE HUYOOOO JANGWANI…..DILI ZIMA LIMEMALIZWA SALAMANDA….

Baleke to Yanga

UONGOZI wa Yanga umeamua kubadilisha maamuzi yao ya kumsajili Jonathan Sowah na karata yao kuelekeza kwa aliyekuwa mshambiliaji wa Simba, Jean Baleke.

Baleke juzi alionekana katika ofisi za GSM jijini Dar es Salaam ikielezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na Rais wa Yanga, Hersi Said kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji.

Imeeleza kuwa tayari nyota huyo amefanya mazungumzo na Rais wa Yanga, Hersi Said kwa ajili ya kukamilisha usajili wake kuimarisha safu hiyo ya ushambuliaji na kuchukuwa nafasi ya Joseph Guede.

Kwa mujibu wa Hersi kuwa msimu huo wanafanya usajili bora, utaifanya Yanga kuendelea kuwa imara zaidi ikiwa malengo yao ni kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Amesema usajili umekamilika na wachezaji walisajiliwa ni mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Gamond (Miguel) kulingana na madhaifu ya kikosi chao.

“Tutaboresha kikosi chetu kiwe bora zaidi ya msimu uliopita nani na nani, naamini kwa kushirikiana na kocha wetu, Miguel Gamondi, tutatengeneza kikosi kitakuwa tishio,” amesema.

Amesema anaamini kila mchezaji ambaye wanamsajili anatambua majukumu yake na wanakuwa bora kwa misimu mitatu mfululizo na wanaendelea kufanya hivyo.

Mshambuliaji huyo ameweka wazi hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea na yupo huru kwa sasa anakaribisha timu yoyote inayohitaji huduma ya mchezaji huyo.

Amesema soka ni kazi yake hachagui wapi anatacheza, yupo tayari kurejea kucheza Tanzania au nchini nyingine endapo kuna timu itapeleka ofa na kuhitaji huduma yake.

“Niko Tanzania kwa ajili ya mapumziko na mchezaji huyo huru sasa, sio Yanga tut imu yoyote inayohitaji huduma yangu nipo tayari kuitumikia kwa msimu mpya wa mashindano,” anasema mshambuliaji huyo.

SOMA NA HII  MAYELE ALIMCHUNGULIA MANULA KABLA HAJAMTUNGUA KWA MKAPA