Home Habari za Yanga Leo CHADRACK BOKA ATUA BONGO USIKU WA MANANE…YANGA YAMFICHA HOTELINI

CHADRACK BOKA ATUA BONGO USIKU WA MANANE…YANGA YAMFICHA HOTELINI

Habari za Yanga leo

SAA chache kabla ya kambi mpya ya Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano kuanza kesho Jumatatu, mabosi wa klabu hiyo wakimpokea beki wa kushoto mpya, Chadrack Boka usiku mnene wa juzi, huku ikikwepa kiunzi kilichowekwa na FC Lupopo aliyokuwa akiichezea msimu uliomalizika hivi karibuni.

Beki huyo aliyetua sambamba na meneja wake akiyokea jiji la Kinshasa, DR Congo amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ni kati ya nyota wapya walioanza kutua nchini kujiandaa na kambi ya maandalizi ya msimu mpya itakayoanza kesho Jumatatu.

Awali kulikuwa na Taarifa za kucheleweshwa kwa ITC yake ya kumuwezesha kusajili kwenye mfumo wa FIFA (TMS), ambapo klabu yake ilizuia kwa lengo la kumlazimisha abakie klabuni hapo.

Inasemekana amechelewa kuwasili nchini Tanzania kwa sababu klabu aliyotoka FC Lupopo haikutaka mchezaji huyo aondoke. Hivyo walikuwa wanaweka ngumu sna kumshawishi abaki ili kuitumikia klabu hiyo.

FC Lupopo wanadai mchezaji huyo ni wao wamekiambia Chama cha soka Nchini DRC (FA) kisitume (ITC) kwenda Yanga SC kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

Mchezaji na menejimenti yake wanapambana kutafuta (ITC) ili awahi kuripoti kambini nchini Tanzania kuanzia July (8).

Mchezaji huyo aliyefanya vizuri katika ligi kuu ya DR Congo sio mchezaji wa FC Lupopo, ni mchezaji wa Real Of Kinshasa alijiunga na FC Saint Eloi Lupopo kwa mkopo.

Yanga SC walishamalizana na klabu yake, FC Lupopo ndio waliochelewesha (ITC) yake.

Ieleweke kwamba Tayari klabu ya Yanga imeshaachana na beki wake wa kushot Joyce Lomalisa, na Boka ndiye mrithi wa Lomalisa.

Klabu ya Yanga hadi sasa imetangaza usajili wa wachezaji wawili\, KIUNGO Clatous Chama ambaye mkataba wake na aajiri  wake wa zamani Simba SC ulimalizika tangu June 30 mwaka 2024, na hawakutaka kumuongeza mkataba mpya, pamoja na Prince Dube ambaye amesajiliwa kama mchezaji huru akijivunjia mkataba na Azam FC.

Wanachokifanya Yanga kwa sasa ni kuwabakiza wachezaji wao tegemezi, na hadi sasa wamewaongeza mikataba wacheza kama Diarra, Mwamnyeto, Fardi Mussa, na Nickson Kibabage.

SOMA NA HII  NAMBA 6 WA YANGA, BEKI AFUNGUKA BALAA LAKE