Home Habari za Simba Leo FELIX SUNZU: SIMBA IMELAMBA DUME…ATOA TAHADHARI KWA MUTALE

FELIX SUNZU: SIMBA IMELAMBA DUME…ATOA TAHADHARI KWA MUTALE

Habari z Simba, Felix Sunzu Kuhusu Joshua Mutale

Straika wa zamani wa Simba, Felix Sunzu akizungumzia usajili wa kiungo mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Joshua Mutale kutoka Zambia amesema kwamba timu hiyo imelamba dume, huku akimuonya asimezwe na presha ya mashabiki ambayo itampoteza na kuangusha matumaini ya timu hiyo.

Mutale ambaye ni miongoni mwa nyota wapya waliotambulishwa na Simba, akisajiliwa kutoka Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu, msimu uliopita alifunga mabao matano na asisti tatu kupitia mechi 26 alizocheza.

Hadi sasa Simba imetambulisha wachezaji 8 Charles Ahoua, Lameck Lawi, Abdulrazak Hamza, Valentino Mashaka,Steven Mukwala, Augustine Okejepha, Deborah Fernandes na Omary Adam sambamba na benchi jipya la ufundi chini ya Fadlu Davids kutoka Afrika Kusini aliyetua na wasaidizi wanne akiwamo Riedoh Beirden aliyewahi kuitumikia Yanga.

Wengine waliotua na Fadlu ni Wilken Darian, Mueez Kajee na Wyne Sandilands wote kutoka Sauzi, huku wachezaji waliotemwa ni Luis Miquissone, Clatous Chama, Saido Ntibazonkiza, Henock Inonga, John Bocco, Kennedy Juma na Idd Shaaban Chilunda, ilhali Kramo Aubin akitolewa kwa mkopo Al Hilal, Sadio Kanoute, Babacar Sarr, Pa Omar Jobe wakielezwa wapo njiani kuachwa.

Sunzu ambaye naye ni Mzambia aliyeweka makazi jijini Mwanza, alisema Mutale ana sifa kama za Emmanuel Okwi kwani ana kasi, uwezo wa kumiliki mpira na kuingia kwenye boksi la wapinzani, hivyo ataweza kupika mabao mengi msimu ujao kama atajiamini.

Alisema mashabiki wa Simba wana shauku na matarajio makubwa kwa mastaa wapya baada ya kupoteza nyota muhimu, hivyo anapaswa kujiamini na kuonyesha uwezo katika mechi tatu za kwanza ili wasimgeuke na kumtoa njiani.

“Unajua mpira wa Tanzania ni mgumu unatakiwa kuchukua gemu tatu kucheza vizuri, akifikiria na kusikiliza mashabiki atapotea, asipowasikiliza ataendelea na mpira wake. Alisema Felix Sunzu.

“Yule dogo anajua mpira. Usipocheza vizuri mechi nne itakuwa ni shida inapoteza kujiamini,” – Felix Sunzu aliyeshiriki ‘mauaji’ ya Yanga ilipopigwa mabao 5-0 katika mechi ya kufungia msimu ya Dabi ya Kariakoo iliyopigwa Mei 6, 2012.”

“Ana kasi, uwezo wa kucheza namba saba na 11, anakimbia kwa kasi kuingia maeneo ya hatari ana sifa kama Emmanuel Okwi vile alikuwa anaweza kutoka pembeni na kuingia ndani. Ana kasi na uwezo wa kupiga chenga, ndivyo alivyo huyu dogo (Mutale).” Alimalizia kusema Felix Sunzu.

SOMA NA HII  CHAMA AKOLEZA 'PILIPILI' ISHU YA MIQUISSONE KURUDI SIMBA...AJIKUTA AKIANIKA KILA KITU HADHARANI...