Home Habari za Simba Leo SIMBA YASHUSHA MCONGO…VIUNGO WAWILI WATAMBULISHWA

SIMBA YASHUSHA MCONGO…VIUNGO WAWILI WATAMBULISHWA

Habari za Simba

KLABU ya Simba imethibitisha kumsajili kiungo mkabaji Debora Fernandes kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Wekundu hao wa Msimbazi akitokea Klabu ya Mutondo Stars ya Zambia, anamudu kucheza kiungo mkabaji na  kiungo mshambuliaji yaani namba nane.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesemw: Kiungo Debora Fernandes, 24, mwenye uraia pacha wa Congo Brazzaville lakini anayechezea timu ya taifa ya Gaboni amejiunga nasi akitokea Mutondo Stars ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu.

“Debora anamudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji ingawa mwenyewe anafurahi kucheza kiungo wa juu yaani namba nane.

“Ujio wa Debora unaongeza nguvu kwenye eneo letu la kiungo kwa kuwa anaweza kuzuia na kupiga pasi sahihi kuelekea mbele na kuanzisha mashambulizi.

“Tunaendelea kusuka timu imara kwa ajili ya muda mrefu ndiyo maana usajili wetu umezingatia umri wa wale tunaowasajili.”

Debora ni mchezaji wa saba mpya kutambulishwa ndani ya Simba kipindi hiki cha usajili baada ya Joshua Mutale, Steven Mukwala, Abdulrazack Hamza, Jean Charles Ahoua, Valentino Mashaka na Augustine Okejepha.

Huku pia mchezaji  wa nane kutambulishwa Simba, ni Omary Adam Omary kutokea timu ya Mashujaa FC ya mkoani  Kigoma,huyu anamuda kucheza nafasi  ya kiungo wa kati kama  namba 8, namba 10 na namba 6.

Klabu hiyo inasajili  wachezaji wenye umri mdogo, hadi sasa usajili wenye umri  mkubwa ni Steve Mukwala ana miaka 24, hii inatoa taswira ya  kuwa na project nzuri ya baadae.

SOMA NA HII  RASMI...AL AHLY WAILAINISHIA SIMBA KWA MIQUISSONE...MABOSI MSIMBAZI WAPAGAWA NA MSHAHARA WAKE...