Home Habari za Yanga Leo PRINCE DUBE ADUI WA SIMBA ATAMBULISHWA YANGA…KIMAFIA ZAIDI

PRINCE DUBE ADUI WA SIMBA ATAMBULISHWA YANGA…KIMAFIA ZAIDI

Habari za Yanga, Prince Dube

Nyota wa zamani wa Highlanders FC ya Bulawayo Zimbabwe ya Mugabe, Alipita Super Sports United ya Pretoria na akatamba pia Black Leopard zote kwa Madiba Hayati Nelson Mandela, Tanzania ya Mwalimu Julius Nyerere alitambulishwa na wahoka mikate wa viunga vya Azam Complex, Azam FC.

HATIMAYE Kimefahamika, Uongozi wa Yanga jana usiku mida ya ssa 6 walimtambulisha mshambuliaji anayeua akitabasamu Mwana Mfalme Prince Dube.

Prince Dube amejiunga nna Ynaga kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru, baada ya kuvunja mkataba wake na waajiri wake wa zamani Azam FC.

Nyota huyo alikuwa akiwapa tabu makipa wengi Bongo ikiwa ni pamoja na wale wa Simba kama Aishi Manula, Ayoub Lakred, Ally Salim walipokuwa wakikutana kwenye mashindano mbalimbali,

Ikumbukwe kwamba matajiri wa Dar, Azam FC walieleza kuwa walipokea ofa kutoka kwa Simba ikihitaji huduma ya Prince Dube wakati mchezaji huyo alipoomba kuvunja mkataba wake.

Prince Dube alivunja mkataba na Azam FC kwa kufuata masharti yaliyokuwa kwenye mkataba wake hivyo alikuwa huru kujiunga na mabingwa wa msimu wa 2023/24 Yanga.

Raia huyo wa Zimbabwe amesaini dili la miaka miwili kuitumikia timu ya Yanga atakutana na Simba ndani ya ligi kwenye Kariakoo Dabi akiwa na uzi wa Yanga.

Msimu wa 2023/24 walipokutana na Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza alifunga bao moja kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na bao la Simba lilifungwa na Clatous Chama ambaye kwa sasa yupo ndani ya Yanga.

Lakini tangu atue ardhi ya Tanzania Prince Dube hajawahi kuibuka mfungaji bora hata mara kwa misimu minne aliyocheza Ligi Kuu ya NBC, huenda kwa kutua Yanga atakuwa mfungaji bira kutokana na safu bora ya viungo iliyopo klabuni hapo.

Kwa sasa safu ya viungo ya Yanga inaunda na Khaleed Aucho, Mudathir Yahya, Maxi Nzengeli, Stephen AZIZ KI, Pacome, Salum Abubakar Sure Boy, na Clatous Chota Chama ambaye naye amesajiliwa akitokea Simba.

SOMA NA HII  NABI AINGIA MCHECHETO NA MBEYA KWANZA....AHOFIA MATOKEO YA SARE INGINE...SIMBA WANAMENDEA...