Home Habari za Yanga Leo GAMNDI AFUNGUKA KUHUSU USAJILI WA YANGA…AOMBA JAMBO MOJA.

GAMNDI AFUNGUKA KUHUSU USAJILI WA YANGA…AOMBA JAMBO MOJA.

Habari za Yanga-Gamondi

KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kuwa anafurahishwa na usajili ambao umefanywa na uongozi wa kuleta MASTAA.

Lakini wanahitaji muda wachezaji Wote wapya kuzoea mazingira ya timu, mbinu na falsafa yake Ili kuweza kupata kile ambacho wanakihitaji.

“Nafurahia kuona usajili huu ambao unafanyika. Wachezaji wazuri ambao wanakuja kutupatia kitu kikubwa zaidi kwenye timu yetu.

“Lakini hata hivyo bado wanahitaji muda ili KUELEWA falsafa, mbinu na mazingira ya timu yetu Ili kuweza kutupatia tunachotaka.”Alisema Gamondi.

Klabu ya Yanga mpaka sasa wamefanikiwa kukamilisha sajili za wachezaji wenye majina makubwa kama Clatous Chama akitokea Simba, ila amesajiliwa kama mchezaji huru.

Pia aliyekuwa mchezaji wa FC Lupopo ya DR Congo Chadrack Boka beki wa kushoto ambaye ni mrithi wa Joyce Lomalisa, na Abubakar kHOMEINY Mlinda mlango mrithi wa Metacha Mnata aliyesajiliwa na Singida Blak Stars.

Na Mwana Mfalme Prince Dube ambaye alivunja mkaaba wake na klabu ya wauza Ice Cream Azam FC.

Wchezaji wengine wanaopewa nafasi ya kuja kujiunga na Yanga kwa msimu ujao ni Jean Baleke ambaye aliwahi kupita Simba, kabla ya kujiunga na Al Ittihad ya Libya ambako alikuwa mfungaji bora.

Baleke anachukua nafasi ya mshambuliaji Jonathan Sowah ambye alikuwa anahusishwa zaidi na Yanga, lakini Uongozi ukaona ukimsajili Jean Baleke basi tatizo lao la washambuliaji litapa suluhisho.

Moja kati ya mastaa waliopo Simba kwa sasa ni Aziz Ki ambaye hivi karibuni alizua sintofahamu baada ya kusemekana bado hajaongeza mkataba na timu yake ya sasa. Ila Jana Julai 10 amethibitisha kwamba aaendelea kukipiga katika klabu hiyo.

SOMA NA HII  MAANA YA NENO SANDA...KWENYE JEZI MPYA ZA SIMBA