Home Uncategorized ISHU YA CHAMA KUIBUKIA YANGA, UONGOZI WA SIMBA WAJIBU NAMNA HII

ISHU YA CHAMA KUIBUKIA YANGA, UONGOZI WA SIMBA WAJIBU NAMNA HII


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kuhusu tetesi za mchezaji wao, raia wa Zambia, Clatous Chama, ambaye anadaiwa kuwa mkataba wake uko karibuni kumalizika hivyo ataondoka klabuni hapo huku akihusishwa kujiunga na Klabu ya Yanga SC.

 

Manara amesema hayo leo leo Septemba 24, alipotembelea Studio za +255 Global Radio akiambatana na Idara ya Habari ya klabu hiyo ndani ya Global Group kwenye ziara ya kikazi yenye lengo la kukuza na kudumisha mahusiano na idara ya habari.

 

“Hii ni mara yangu ya tatu kutembelea media houses Tanzania tangu niingie kwenye kazi hii, tumekuja kuwaeleza mashabiki wetu na Watanzania mambo ambayo Simba SC tumepanga kuyafanya.

 

“Viongozi wa Simba SC wataongea na uongozi wa Clatous Chama kuangalia namna ya kuongeza mkataba wake ambao unaisha Julai 2021, nimesikia Yanga SC wanasema watamchukua, pale atacheza na nani? Pasi za visigino atampa nani?


“Ili Chama aweze kucheza vizuri anahitaji timu inayomiliki mpira, akienda Yanga SC atachezaje? Kwanza hawana pesa ya kumnunua, mkataba wake ni dola milioni moja, Yanga wana hiyo pesa? Mashabiki wa Simba SC wasibabaishwe na propaganda za mitandaoni, viongozi wana uchungu na timu hawawezi kuruhusu aondoke,” amesema.

 

SOMA NA HII  MOHAMED SALAH NI WA MOTO EPL, ARSENAL HAWANA BAHATI NAYE KABISA