Home Habari za michezo SMBA, YANGA KUWAJUA WAPINZANI WAO LEO KIMATAIFA.

SMBA, YANGA KUWAJUA WAPINZANI WAO LEO KIMATAIFA.

HABARI ZA MICHEZO, SIMBA NA YANGA

DROO ya Ligi  ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika itachezeshwa leo Cairo Misri, kujua ni timu zipi zitacheza hatua ya awali ya michuano yote.

Yanga na Azam FC wanakipiga Ligi ya Mabingwa, na Simba na Coastal Union zikicheza Kombe la Shirikisho ikiwa ni mara ya kwanza kwa wagosi wa kaya kushiriki michuano hiyo licha ya kuwahi kufanya vizuri miaka ya nyuma katika Ligi kuu.

MFUMO   WA UPANGAJI DROO UKOJE?

Kwa mujibu wa mfumo wa CAF kwenye klabu bingwa Afrika kupanga mechi za awali wana jumla ya makundi matatu, ambapo kuna timu tano ambazo hazitocheza hatua ya awali ( Preliminary) timu hizo ni Al Ahly, Esperance, Mamelodi, Petro na TP Mazembe.

Kisha kuna timu nne (4) ambazo zinatambuliwa kama HIGHEST RANKED yaani ziko na alama nyingi kwenye mfumo wa CAF ambazo timu hizo ni YANGA 🇹🇿, Pyramids, Raja na CR Belouzdad.

Kiufundi ukichukua hizo timu tano za juu kisha ukijumlisha na hizo nne basi unaenda kupata jibu ya timu bora Afrika kwa mujibu wa CAF kwenye klabu bingwa Afrika, Premier Club Competitions.

Lakini bado Yanga ataanzia hatua za awali sambamba na hao wenzake watatu, ni timu tano tu hazitoanzia hatua za awali.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali zipo 12 ambazo ni;

SIMBA SC- Tanzania

RS BERKANE- Morocco

FC LUPOPO- DR Congo

STADE MALIEN- Mali

ENYIMBA FC-Nigeria

ASEC MIMOSAS- Ivory Coast

ZAMALEK SC- Misri

USM Alger- Algeria

AS Vita- DR Congo

SHEKUKHUNE FC- Zambia

EL MASRY- Misri

CS Sfaxien- Tunisia

SOMA NA HII  AHMED ALLY ATANGAZA VITA...SIMBA IMEKAMILISHA USAJILI.