Home Habari za Simba Leo SIMBA YANGA KUKIPIGA NA AL MERREIKH, TP MAZEMBE CECAFA.

SIMBA YANGA KUKIPIGA NA AL MERREIKH, TP MAZEMBE CECAFA.

Habari za Michezo leo

Timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya Kimataifa, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika zitapata nafasi nzuri ya kujiandaa na msimu mpya kwa kucheza na timu za Zambia, Sudan, Rwanda, Kenya na Uganda.

Habari za uhakika ni kwamba Yanga, Azam, Simba na Coastal Union zitashiriki michuano ya Cecafa dhidi ya timu kutoka katika mataifa hayo.

Cecafa ni Baraza lenye wanachama 12 ikiwemo Zanzibar.

Timu hizo nne zitakazoshiriki Caf Champions na Caf Confederation Cup zitacheza dhidi ya Al Hilal, Al Merreikh na Hai Ak Wadi za Sudan, Red Arrow ya Zambia na TP Mazembe ya DRC.

Michuano hiyo ambayo itakuwa kabla ya kuanza kwa msimu mpya zitashirikisha timu 16 na itapigwa Tanzania.

Timu nyingine ni Nyasa Big Bullets ya Malawi, SC Villa ya Uganda, APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Vital’O (Burundi), JKU (Zanzibar) na El Merreikh Bentiu (Sudan Kusini.)

Mashindano hayo yalisimama kwa miaka mingi kabla ya kutangazwa kurudi tena mwaka huu, yakipewa nguvu zaidi na Serikali ya Uganda na Tanzania, abapo mwaka jana Rais Samia Suluhu Hassan alidhamini mashindano hayo kwa ngazi ya wanawake.

Huenda vilabu vya Tanzania vikapata muda wa kucheza mechi hizi na kuzitumia kama Pre Season yao,  hivyo wanahitaji kukamilisha usajili wao mapema kwani ratiba ya mashindano kwa msimu ujao inaonekana kuwa nguvu zaidi.

SOMA NA HII  CLATOUS CHOTA CHAMA NDANI YA MBIO ZA KUWANIA MCHEZAJI BORA CAF CHAMPIONSHIP