Home Habari za Simba Leo SIMBA SIO KINYONGE…WANA REKODI HII NZURI

SIMBA SIO KINYONGE…WANA REKODI HII NZURI

Habari za Simba leo

SIMBA SC licha ya kugotea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na kusepa na tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiungana na Coastal Union ya Tanga.

SIMBA SC iliyomaliza msimu ikiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, huenda ulikuwa msimu mbaya zaidi kwao lakini hawakuwa kinyonge kiasi hicho, wana rekodi hii nzuri zaidi ambayo haijazungumzwa sana.

Simba inaingia kwenye timu yenye rekodi ya kufunga bao kwenye kila mchezo ndani ya ligi msimu wa 2023/24 licha ya kugotea ikiwa nafasi ya tatu.

Katika mechi 30 ambazo ilicheza timu hiyo safu yake ya ushambuliaji ilifunga jumla ya mabao 59 ikiwa ni namba tatu pia kwa timu ambazo zimefunga mabao mengi kwenye ligi.

Namba moja ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambayo ilimaliza msimu ikiwa na mabao 71 kinara wa utupiaji akiwa ni Aziz KI aliyefunga jumla ya mabao 21 ndani ya ligi.

Aziz Ki ni mkali wa mguu wa kushoto ambapo alitumia mguu huo kufunga mabao 17 na mabao matatu alifunga kwa kutumia mguu wa kulia na bao moja alifunga kwa pigo la kichwa ilikuwa dhidi ya Tabora United mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  MAYELE AWEKA REKODI HII YANGA...APEWA JEZI YA HESHIMA...ISHU NZIMA IKO HIVI