Home Habari za Simba Leo AHMED ALLY ATANGAZA VITA…SIMBA IMEKAMILISHA USAJILI.

AHMED ALLY ATANGAZA VITA…SIMBA IMEKAMILISHA USAJILI.

Habari za Simba leo

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuwa michakato ya usajili inaendelea na wako katika hatua za mwisho kukamilika

Baada ya kutoa Thank You kwa wachezaji watano pamoja na kutangaza usajili wa beki Lameck Lawi, ukimya umetawala Msimbazi jambo lililowapa hofu baadhi ya Wanamsimbazi wenye shauku kubwa ya kutaka kufahamu maboresho ya kikosi

“Usajili unaendelea, mpaka sasa umekamilika kwa asilimia kama 97 hivi, hivyo mashabiki wasione kama tuko kimya, tunakamilisha ujenzi wa nyumba yetu”

“Kuanzia wiki ijayo tutaanza kutangaza wachezaji wote tuliowasajili, itakuwa bandika- bandua bila ya kupumzika”

“Najua shauku ya Wanamsimbazi lakini niwahakikishie tumeleta vyuma kwelikweli. Baadhi ya wachezaji tayari wameshatua kwa ajili ya taratibu za maandalizi ya pre-season,” alisema Ahmed

Simba inatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo kuelekea Misri kwa ajili ya pre-season itakayodumu kwa wiki tatu na kikosi kurejeea kwa ajili ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika August 03.

Hadi sasa Simba imemalizana na wachezaji kadhaa wa kimataifa na wa ndani, huku wanaopewa nafasi zaidi ya kutambulishwa mapema, ni winga wa Power Dynamos Joshua Mutale, Steve Mukwala, Augustine Okejepha, Valentina Nouma, Debora Fernandes.

Huk kwa upande wa wazawa Simba imetambulisha mchezaji mmoja tu Lameck Lawi kutoka Coastal Union, ambaye nae amezua mgogoro  wa kimkataba na waajiri wake wa zamani wakidai Simba ilichelewesha malipo hivyo dili lilifutwa.

SOMA NA HII  SABABU ZA KOCHA WA VIUNGO YANGA KUONDOKA...GAMONDI AHUSISHWA