Home Habari za Yanga Leo HUKUMU YA YANGA YAZUA BALAA…MAGOMA AFUNGUKA URAIS WA HERSI

HUKUMU YA YANGA YAZUA BALAA…MAGOMA AFUNGUKA URAIS WA HERSI

habari za yanga-MAGOMA YANGA

Yanga imepokea hukumu ya kutotambulika kwa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo kufuatia hukumu iliyotolewa Agosti 2, 2023 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kwa mujibu wa Mwananchi wenye nakala ya Hukumu hiyo inatokana na kesi ya msingi iliyofunguliwa Agosti 4, 2022 na walalamikaji Juma Ally na Geoffrey Mwaipopo, wakitaka kutotambulika kwa Baraza la wadhamini la Yanga lililowekwa madarakani kwa katiba ya mwaka 2010, kukosa sifa kisheria.

Aidha, walalamikaji pia walitaka miamala yote ya fedha iliyoidhinishwa na baraza hilo, kutotambulika kisheria kwa kuwa ni batili.

Hukumu hiyo, imeitaka bodi iliyokuwa madarakani kwa katiba ya mwaka 1968 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2011, kurudi madarakani kuongoza klabu ya Yanga.

Inaelezwa walalamikaji walirudi mahakamani kukazia hukumu hiyo kuiondoa madarakani bodi hiyo wadhamini ndipo uongozi wa Sasa wa Yanga ukapenyezewa taarifa.

Baraza linalolamikiwa linaongozwa na Mwenyekiti George Mkuchika na wajumbe wake Mama Fatma Karume, Dk Mwigulu Nchemba, Tarimba Abbas na Antony Mavunde.

Ingawa viongozi wa juu wa Yanga hawakupatikana kufafanua hukumu hiyo lakini Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Wakili Simon Patrick amekiri klabu yao kupokea taarifa hiyo.

Simon, amesema Yanga inafuatilia hukumu hiyo ambayo tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo klabu yao haikuwa inajua lolote kabla ya Sasa kupokea wito wa kuitwa mahakamani.

“Nikweli Kuna hiyo hukumu lakini niseme kuanzia kufunguliwa kwa kesi hiyo, Yanga haikuwa na taarifa yoyote na hata hukumu ilipotoka pia hatukuwa tunafahamu,”amesema Patrick.

“Tumechukua hata jitihada za kuwatafuta hao walalamikaji kama ni wanachama wa klabu yetu, hatuoni taarifa zao kwenye orodha ya wanachama wetu halali wa klabu,” aliongeza kusema wakili huyo.

“Kama tungefahamu tungechukua hatua za hata kuitetea klabu lakini kwa sasa tunafanya juhudi za kujua undani wake na ikiwezekana kwa kuwa walalamikaji wamerudi mahakamani kukazia hukumu na sisi tutaangalia nafasi ya kukata rufaa kwa kuwa klabu haikuwa inafahamu lolote na Ina haki ya kusikilizwa.

BAADA ya beki wa kati Mganda Gift Fred kudaiwa kwamba amekosa namba kwenye kikosi cha Yanga, hivi sasa inaelezwa timu hiyo itamtoa kwa mkopo kwenda kwa mabingwa wa Rwanda, APR.

Beki huyo alijiunga na Yanga wakati wa usajili wa dirisha kubwa, Julai 7, mwaka jana, akitokea SC Villa ya Uganda, lakini inaelezwa atatolewa kwenda Rwanda kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha wakali wa Jangwani.

Mkataba wa beki huyo na Yanga unatamatika Juni 2026 na inaelezwa kwamba timu hiyo haina mpango wa kuendelea naye baada ya eneo hilo kutawaliwa na wazawa ambao wanafanya vizuri. Wazawa wanaotesa eneo la ulinzi wa kati ni Ibrahim Abdullah ‘Bacca’, Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job.

Pamoja na mambo mengine kuondoka kwa Gift kutaipa Yanga nafasi ya kusajili mchezaji mwingine wa kigeni baada ya idadi ya wachezaji 12 kutimia.

Hadi sasa klabu ya Yanga imefanya sajili za wachezaji 6, ikiwemo wa 5 wa Kimataifa huku ikihitaji kumuongeza Jean Baleke katika kuimarisha eneo lao la ushambuliaji.

Baada ya kuwasili Yanga Gift Fred hakuwa anapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara, na mara nyingi alikuwa akikaa benchi tu au kupewa muda mchache wa kucheza.

Sababu kubwa ni uwepo wa mabeki wenye uwezo mkubwa kumzidi Gift huku, Yanga ikizidi kuwaamini mabeki wazawa zaidi katika safu yao ya ulinzi.

Msimu huu Yanga itaachana na Zawadi Mauya pia ambaye alikuwa ancheza kiungo cha ulinzi, huku pia ikiwa imeshaachana na Metacha Mnata mlinda mlango wao aliyetimkia katika klabu ya Singida Black Star.

SOMA NA HII  ALOO SIMBA NA YANGA NDANI NTITI NJE NTITI...VIKOSI VYOTE VYA MOTO