Home Habari za Yanga Leo MGANDA WA YANGA AKATWA KICHWA…KUSAJILIWA MWINGINE WA KIGENI

MGANDA WA YANGA AKATWA KICHWA…KUSAJILIWA MWINGINE WA KIGENI

Habari za Yanga leo

BAADA ya beki wa kati Mganda Gift Fred kudaiwa kwamba amekosa namba kwenye kikosi cha Yanga, hivi sasa inaelezwa timu hiyo itamtoa kwa mkopo kwenda kwa mabingwa wa Rwanda, APR.

Beki huyo alijiunga na Yanga wakati wa usajili wa dirisha kubwa, Julai 7, mwaka jana, akitokea SC Villa ya Uganda, lakini inaelezwa atatolewa kwenda Rwanda kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha wakali wa Jangwani.

Mkataba wa beki huyo na Yanga unatamatika Juni 2026 na inaelezwa kwamba timu hiyo haina mpango wa kuendelea naye baada ya eneo hilo kutawaliwa na wazawa ambao wanafanya vizuri. Wazawa wanaotesa eneo la ulinzi wa kati ni Ibrahim Abdullah ‘Bacca’, Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job.

Pamoja na mambo mengine kuondoka kwa Gift kutaipa Yanga nafasi ya kusajili mchezaji mwingine wa kigeni baada ya idadi ya wachezaji 12 kutimia.

Hadi sasa klabu ya Yanga imefanya sajili za wachezaji 6, ikiwemo wa 5 wa Kimataifa huku ikihitaji kumuongeza Jean Baleke katika kuimarisha eneo lao la ushambuliaji.

Baada ya kuwasili Yanga Gift Fred hakuwa anapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara, na mara nyingi alikuwa akikaa benchi tu au kupewa muda mchache wa kucheza.

Sababu kubwa ni uwepo wa mabeki wenye uwezo mkubwa kumzidi Gift huku, Yanga ikizidi kuwaamini mabeki wazawa zaidi katika safu yao ya ulinzi.

Msimu huu Yanga itaachana na Zawadi Mauya pia ambaye alikuwa ancheza kiungo cha ulinzi, huku pia ikiwa imeshaachana na Metacha Mnata mlinda mlango wao aliyetimkia katika klabu ya Singida Black Star.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA SAFARINI KUELEKEA MOROCCO...WATUMIA MBINU HII KUWACHANGANYA WAARABU