Home Habari za Simba Leo CHAMA, DUBE, ABUYA, BALEKE WAIPA SERIKALI MAMILIONI

CHAMA, DUBE, ABUYA, BALEKE WAIPA SERIKALI MAMILIONI

HABARI ZA YANGA-GAMONDI

Uhamisho wa wachezaji wa kimataifa wa Yanga, Cleatus Chama, Prince Dube na Duke Abuya utainufaisha serikali mamilioni ya fedha.

Msajili wa Vyama vya Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Evordy Kyando amesema kuwa sababu ya kiwango cha uhamisho wa ndani kuwa kikubwa kuliko uhamisho wa nje kuja ndani ni gharama kutofautiana.

Kwa maana hiyo uhamisho wa wachezaji watatu wa Yanga tu Chama aliyetoka Simba, Dube aliyotoka Azam na Abuya aliyetoka Singida utaipa serikali zaidi ya sh milioni nane.

Lakini pia uhamisho wa kimataifa nao utawaingiza fedha zaidi.

Klabu ya Yanga hadi saa imetambulisha wachezaji wapya 5, ambapo Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Abubakar Khomeiny Mlinda mlango, Kiungo Duke Abuya na Azizi Andabwile.

Kwa upande wa Simba yenyewe haijafanya uhamisho wa wachezaji wa kigeni wa ndani, lakini imesajili wachezaji wengi zaidi ya kawaida, kuna Jean Charles, Steve Mukwala, Joshua Mutale, Deborah Fernandes, Augustine Okejepha, Chamou Karaboue, Valentino Nouma.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AIMALIZA YANGA KABLA YA KUINGIA DIMBANI, LEO NDIO KAZI IPO HIVI