Home Habari za Yanga Leo JOSEPH AMUACHIA BALEKE NAMBA… YANGA YAMPA THANK YOU

JOSEPH AMUACHIA BALEKE NAMBA… YANGA YAMPA THANK YOU

Habari za Yanga- Joseph Guede

MABOSI wa Singida Black Stars hawataki utani ambapo kwenye safu ya ushambuliaji wamemuongeza mtambo wa mabao Joseph Guede ambaye msimu uliopita wa 2023/24 alikuwa ndani ya Yanga.

Utambulisho wake ndani ya Singida Black Stars utaongeza kitu kwenye eneo la ushambuliaji ukizingatia kwamba msimu mpya wa 2024/25 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ikumbukwe kwamba Guede raia huyo wa Ivory Coast, amefunga mabao sita (6) na assist mbili kwenye NBC Premier League, akitumia dakika 1,032 kwenye mechi 17 alizocheza.

Kwenye CRDB Bank Federation Cup, Guede amefunga mabao mawili kwenye mechi tano alizocheza akitumia dakika 118. Anaanza changamoto mpya kwenye timu mpya msimu wa 2024/25 na amempisha Mshambuliaji wa DR Congo Jean Baleke.

Ipo wazi kwamba anaingia kwenye orodha ya wachezaji waliofunga bao muhimu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Mkapa na timu hiyo ikatinga hatua ya robo fainali 2023/24.

Akiwa na Yanga katwaa mataji mawili makubwa la ligi na CRDB Federation Cup anakuwa chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems wengi wanapenda kumuita Uchebe.

Klabu ya Yanga imesajili wachezaji kibao wenye majina mkubwa na uwezo uwanjani,  kuna Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Aziz Andabwile, na sasa Duke Abuya.

Wachezaji wanaohusishwa zaidi kujiunga na Simba, ni Jean BALEKE aliyewahi kucheza Simba kwa msimu mmoja na nusu akifunga jumla  ya mabao 16, kisha akatimkia kwenda klabu ya Al Ittihad ya Libya.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUPATA USHINDI JANA...NABI AWADINDIA MASHABIKI...AFUNGUKA NAMNA ALIVYOTAKA MAMBO YAWE...