Home Habari za Yanga Leo YANGA YAANZA NA GUEDE…AMPISHA MGHANA & BALEKE

YANGA YAANZA NA GUEDE…AMPISHA MGHANA & BALEKE

Habari za Yanga leo

MSHAMBULIAJI aliyemaliza na mabao sita katika Ligi Kuu Bara na matatu ya Kombe la FA na moja la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita akiwa na kikosi cha Yanga, Joseph Guede huenda akaendelea kusalia nchini licha ya kudaiwa kupewa ‘thank you’ Jangwani, baada ya kudaiwa anajiandaa kutua Singida Black Stars.

Guede alijiunga na Yanga katika dirisha dogo la Januari akitokea Tuzlaspor FC ya Uturuki akiitumikia kwa miezi sita na anatajwa ni kati ya nyota wa kigeni walioachwa kikosini, ili kupisha mastaa wapya akiwamo Jean Baleke anayeenda kuchukua nafasi yake eneo la ushambuliaji.

Katika eneo la ushambuliaji la Yanga tayari wameanza kushusa vyuma vya maana, wamemtambulisha Prince Dube ambaye, alivunja mkataba wake tangu mwezi Machi na waajiri wake a zamani Azam FC.

Yanga wamemsajili kama mchezaji huru baada ya kumaliza kulipa fidia ya mkataba wake, Utambulisho wa mchezaji huyo unatoa ishara ya mkono wa kwaheri kwa Joseph Guede.

PIA mbali na aliyekua mshambuliaji wa Simba na Al Ittihad ya Libya Jean Baleke kuhuishwa na Yanga, tayri kumekuwa na taarifa za mchezaji mwingine wa Ghana kutoka klabu ya Medeama Jommathan Sowah anapewa nafasi nyingine ya kukamilisha nafasi ya ushambuliaji.

Msimu uliopita Yanga ilifanikiwa kutoa mfungajji bora wa Ligi Kuu ya NBC ambaye sio strika kwa asili ila ni kiungo wa ushambuliaji, Stephen Aziz Ki aliyemaliza Ligi na Magoli 22 nyuma yake akifuatiwa na Feisal Salum Abdallah Fei Toto, aliyejiunga na Azam FC akitokea hapo hapo yanga.

Hadi sasa Yanga imetambulisha wachezaji 2, Prince Dube, na Clatous Chama, huk ikiwaongeza mikataba wachezaji wake tegemezi kama Nickson Kibabage, Bakari Mwamnyeto, Djigui Diarra, na Farid Mussa, AbdulTwalib Mshery.

Huku ikielezwa wamewapa mkono wa kwaheri baadhi ya nyota wake Zawadi MAUYA, Augustine Okrah, Metacha Mnata, Skudu Makudubela na Joseph Guede.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF NA WAALGERIA....MASTAA 'WASUKWA' KIULAYA ULAYA...