Home Habari za Yanga Leo MAHAMAKAMA YAKUBALI OMBI LA YANGA…KESI YAO KUSOGEZWA MBELE

MAHAMAKAMA YAKUBALI OMBI LA YANGA…KESI YAO KUSOGEZWA MBELE

Habari za Simba- Simon Patrick

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imekubali ombi la klabu ya Yanga ya kusogezwa mbele kwa muda wa kusikilizwa kesi iliyofunguliwa na wanachama wa klabu hiyo kuhusu uhalali wa Baraza la wadhamini wa klabu hiyo

Awali Mahakama hiyo iliamuru Uongozi wa klabu ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye klabu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.

Kufuatia hatua hiyo Mahakama hiyo itaisikiliza upya kesi hiyo na baadae maamuzi yatatolewa kuhusu kesi hiyo.

Sakata hilo lilimfikia Waziri wa Utamaduni na Michezo Dkt Damas Ndumbaro na kuwashauri Viongozi wa Yanga kutumia njia sahihi kutatua mgogoro wao.

“Mimi niwashauri viongozi na wanachama wa Yanga, migogoro haina tija na inarudisha nyuma maendeleo.

“Pia inawaondoa katika ‘reli’ ya kufanya maandalizi ya timu yenye jukumu kubwa la kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa ya CAF),” alisema Waziri huyo na kuongeza;

“Nawashauri wakae meza moja na kutatua, endapo kila mmoja atakuwa anazungumzia kona yake, itachukua muda kumaliza. Wanachotakiwa sasa ni kufanya mjadala wa pamoja na wajue namna ya kumaliza changamoto hiyo. Hii ndiyo njia bora na sahihi zaidi.” Alisema Ndumbaro.

Waziri huyo ambaye ni Mwanasheria pia, aliwakumbusha viongozi wa Yanga na klabu nyingine kufuata taratibu za kisheria wanapofanya mabadiliko ya uongozi kwa mujibu wa katiba.

“Pia viongozi wanatakiwa kufuata sheria, kanuni, taratibu au maagizo yaliyowekwa (Compliance).

“Ni wakati wa klabu kufanya kazi zake kwa kufuata masharti na miongozo iliyowekwa na mamlaka husika. Ni muhimu kwa viongozi wa klabu zote. Hii itasaidia kuondoa matatizo kama haya,” alisisitiza Ndumbaro.

Alisema taratibu zipo wazi, lakini inaonekana kufuatwa inakuwa shida, jambo linalotoa mwanya kwa watu wengine kufanya wanayoona yanafaa.

SOMA NA HII  SIMBA YASHUSHA MRITHI WA INONGA...CHAMOU KARABOUE...BALAA LAKE NI HILI