Home Habari za Yanga Leo MAPYA YAIBUKA…SAKATA LA AZIZI K YANGA..HERSI AFUNGUKA

MAPYA YAIBUKA…SAKATA LA AZIZI K YANGA..HERSI AFUNGUKA

HABARI ZA YANGA, Aziz Ki

Rais wa Yanga, Mhandishi Hersi Said amesema hadi sasa kiungo wa klabu hiyo, Stephen Aziz Ki hajasaini mkataba mpya na kwamba mazungumzo yanaendelea na anaamini kwamba watafikia mwafaka.

Injinia Hersi amesema hayo akifanya mahojiano nchini Afrika Kusini ambapo amekiri kuwa kuna klabu nyingi zinataka kumsajili nyota huyo na kwamba itakuwa ni huzuni kwao kumpoteza raia huyo wa Burkina Faso kwani bado wanahitaji huduma yake.

“Mazungumzo yanaendelea, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kubaki [Yanga] lakini hatujafikia mwafaka,” amesema Hersi akiongeza kuwa Aziz Ki “anataka kubaki Yanga lakini mpira ni biashara siku hizi, hivyo anaweza akatamani kubaki lakini masuala ya kifedha yakamshawishi vinginevyo.”

Amesema kuwa alipomsajili Stephen Aziz Ki miaka miwili iliyopita alimweleza malengo yake ya kuiinua klabu hiyo, na kwamba nyota hiyo ni sehemu muhimu ya mageuzi ambayo yanaendelea ndani ya Jangwani.

Hivi karibuni ikumbukwe tuliripoti sakata la Aziz Ki kuikazia Yanga kusaini mkataba mpya, huku akitaja mahitaji yake il asinye tena.

Inaelezwa kwamba Kiungo huyo ambaye ni MVP wa misimu wa mwaka juzi na Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ulioisha, ametaka kiasi cha USD 20000, sawa na Tsh Milioni 54 kama mshahara wake kwa mwezi.

Pia mchezaji huyo ameendelea kuhitaji dau lake la usajili liongezwe, huku akitaka nyumba nzuri ya kuishi na gari la kutembelea.

Hadi sasa Uongozi wa Yanga unapambana sana kumbakiza Stephen Aziz Ki, huku yeye mwenyewe akiwaahidi Wananchi kuwa ataendelea kusalia klabuni hapo kutumiza malengo ya Yanga ambayo alikubaliana na Injinia Hersi alipokuwa anasinya kandarasi ya kuitumikia Yanga.

Habari hizi zimepokelewa kwa dhana tofauti mitandaoni, wapo wanaoamini kwamba ni kweli Aziz Ki hajasaini mkataba mpya, huku wengine wakiamini kuwa habari hizo ni Propaganda na kinachofannyika ni kutengeneza mazingira ili ionekane Yanga wametumia nguvu kubwa na pesa nyingi kumbakiza Aziz Ki.

SOMA NA HII  SAKATA LA KIFUNGO CHA MANARA...WANASHERIA WA MAHAKAMA WAIBUKA NA HOJA HIZI NONDO...WADAI INAWEZEKANA VIPI...