Home Uncategorized BEKI KISIKI WA YANGA HATIHATI KUIKOSA TANZANIA PRISONS

BEKI KISIKI WA YANGA HATIHATI KUIKOSA TANZANIA PRISONS

 
BEKI  kisiki wa Yanga, Lamine Moro, huenda akaukosa mechi za mwanzo wa msimu kutokana na jeraha la goti alilolipata hivi karibuni kwenye mazoezi ya timu hiyo.

 

Lamine alikuwa kwenye sehemu ya kikosi cha kwanza cha Yanga msimu uliopita huku akiwa mmoja kati ya wachezaji wa kimataifa waliobaki kikosini sambamba na kipa Farouk Shikhalo na kiungo Haruna Niyonzima.

 

Beki huyo amesema kuwa hali yake ya kiafya sasa hivi sio nzuri, japo alitamani sana kuanza msimu na wenzake lakini kutokana na sababu za kiafya ndio maana imebidi kukaa pembeni kujiuguza kwanza.

 

“Nilitamani sana kuanza msimu na wenzangu ila kwa sababu za kiafya sina budi kukaa nje, daktari ameniambia kuwa, nitarejea hivi karibuni lakini nasubiri vipimo zaidi ambavyo natarajia kupimwa wiki ijayo,” alisema Lamine.

 

Yanga msimu huu katika eneo la ulinzi wa kati ina mabeki wanne ambao ni Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Said Makapu na Lamine Moro.


Hakuwa sehemu ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir uliochezwa Uwanja wa Taifa ambapo nafasi yake alicheza Mwamnyeto wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.


Mchezo wa kwanza wa ligi kwa Yanga itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 6 majira ya saa 1:00 usiku.

Chanzo: Championi

SOMA NA HII  PAUL NONGA AGOMEA KUREJEA LIPULI