Home Habari za Yanga Leo MAYELE AZIDI KUWAPASUA KICHWA YANGA.

MAYELE AZIDI KUWAPASUA KICHWA YANGA.

Habari za Michezo

BAADA ya Kuondoka kwa Mzee wa Kutetema Fiston Kalala Mayele kwenye Kikosi cha Young Africans, klabu hiyo imekuwa ikiteseka sana kusaka mbadala au mrithi sahihi wa mshambuliaji huyo.

Klabu ya Yanga wameshasajiliwa washambuliaji sita (6) ili kuziba pengo lake na bado wanasaka mbadala sahihi wa Mkongomani huyo.

Wachezaji ambao waliosajiliwa kuziba pengo la Mayele kwa vipindi tofauti tangu mwamba atimkie kwa waarabu wa FC Pyramids.

1- Hafiz Konkoni >> Hayupo
2- Joseph Guede >> Hayupo
3- Clement Mzize
4- Kennedy Musonda
5- Prince Dube
6- Jean Baleke.

Wachezaji sita hao dhidi ya Kalala mmoja, bado anasakwa mrithi wake na wawili tayari wameaga shindano, ni sahihi kusema wamefeli?

Viatu vya King Mayele vimekuwa vizito sana mpaka sasa kutoka kwenye eneo lake la asili (striker) tunasubiri kuona Prince Dube kama vitamtosha viatu hivyo, ijapo Clement Mzize anajitahidi sana kwa nafasi yake.

Sio tu Dube bali hata washambuliaji wengine kama Baleke, Musonda ambaye amewasili kambini siku ya leo Julai 15, akitokea mapumzikoni.

Hadi sasa Yanga imewatambulisha wachezaji kadhaa akiwemo Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka na Abubakar Khommeiny ambaye ni mlinda mlango, na Aziz Andabwile na Duke Abuya.

Wengine wameongezewa mikataba yao Yanga, Farid Mussa, AbdulTwalib Mshery, Kibwana Shomari, Djigui  Diarra, Aziz Ki Stephen,  Bakari Nondo Mwamnyeto.

Yanga n mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC wanahitajji pia kutetea mataji yao muhimu.

SOMA NA HII  YANGA YAMUWAHI DIARRA CHAP...KUMPA MKATABA NA MSHAHARA MNONO