Home Habari za Simba Leo BREAKING NEWS…CEO SIMBA ANG’ATUKA…MO DEWJI ASAKA MRITHI

BREAKING NEWS…CEO SIMBA ANG’ATUKA…MO DEWJI ASAKA MRITHI

Habari za Simba- Kajula

JULAI 13 Soka La Bongo tuliripoti juu ya hatma ya Mkurugenzi Mtendaji wa Simba Imani Kajula kuwa yuko mbioni kuondoka, sasa ni rasmi Uongozi wa klabu hiyo umetangaza kuachana na CEO wao.

Taarifa iliyotoka Simba inasema kwamba, Kajula atamaliza muda wake Agosti 31 mwaka huu, na hapo atatafutwa CEO mpya.

“Klabu ya Simba inapenda kuujulisha umma kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba imeridhia maombi ya Afisa Mtendaji Mkuu Imani Kajula kuomba kuondoka ifikapo mwisho mwa mwezi Agosti 2024 mkataba wake utakapoisha.

“Kufuatia maamuzi hayo, Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba inafanya jitihada za kupata Afisa Mtendaji Mkuu mpya. Umma utapewa taarifa zoezi hili litakapokamilika.

“Pamoja na uamuzi huu, Afisa Mtendaji Mkuu Imani Kajula anaendelea na majukumu yake ya kiutendaji kikamilifu hadi tarehe 31 Agosti 2024.” Taarifa ya Simba.

Soka la Bongo tunatambua kwamba, Simba imeshawasiliana na Aliyewahi Makama Mwenyekiti wa Klabu ya APR ya Rwanda Uwayezu Francois Regis ili kuchukua nafasi ya Imani Kujula.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa mazungumzo na Francois yamefika hatua nzuri kilichobaki ni kufikia muafaka wa kumalizana naye ili aweze kuipngoza Simba.

Francois, kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa APR ya Rwanda na amewahi pia kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Rwanda (FERWAFA).

“Kajula anakamilisha mkataba wake tu ndani ya Simba lakini makubaliano ya kumalizana endapo mkataba ukiisha yamefanyika na ndio maana uongozi umeamua kufanya mazungumzo na Francois ili kuchukua nafasi yake,” kilisema chanzo hicho.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Simba kuwa na CEO kutoka nje ya nchi, kwani awali iliwahi kumuajiri, Senzo Mbatha kutoka Afrika Kusini ambaye baadaye alijiondoa na kutua Yanga kabla ya kurithiwa na Mzambia, Andre Mtine aliyetokea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.

SOMA NA HII  YANGA KUIKABILI VITA'O NA TAHADHARI HII