Home Habari za Yanga Leo MRITHI WA LOMALISA ATAMBULISHWA YANGA…CHADRACK BOKA YUPO AVIC

MRITHI WA LOMALISA ATAMBULISHWA YANGA…CHADRACK BOKA YUPO AVIC

Habari za Yanga, Chadrack Boka

Yanga imethibitisha kukamilisha usajili wa mlinzi wa kushoto Chadrack Boka kutoka klabu ya FC Lupopo ya DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili.

Ilikuwa ni suala la muda kwa Yangaa kumtambulisha Chadrack Boka aliyetua kuchukua nafasi ya Joyce Lomalisa ambaye kwa sasa anapewa nafasi kubwa ya kujiunga na Namungo FC kutoka mkoani Lindi.

Boka alikuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha FC Lupopo na pia amepata nafasi ya kuitumikia timu ya Taifa ya DR Congo katika michuano ya CHAN.

Unaweza kusema Yanga imetoa chuma upande wa kushoto na imeshusha chuma kwelikweli.

Boka mwenye umri wa miaka 24 anasifika kwa kasi ya kupandisha mashamulizi na umahiri katika ulinzi.

Anakuwa mchezaji wa tatu kutambulishwa katika dirisha hili baada ya Clatous Chama na Prince Dube.

Awali kulikuwa na Taarifa za kucheleweshwa kwa ITC yake ya kumuwezesha kusajili kwenye mfumo wa FIFA (TMS), ambapo klabu yake ilizuia kwa lengo la kumlazimisha abakie klabuni hapo.

Inasemekana amechelewa kuwasili nchini Tanzania kwa sababu klabu aliyotoka FC Lupopo haikutaka mchezaji huyo aondoke. Hivyo walikuwa wanaweka ngumu sna kumshawishi abaki ili kuitumikia klabu hiyo.

FC Lupopo wanadai mchezaji huyo ni wao wamekiambia Chama cha soka Nchini DRC (FA) kisitume (ITC) kwenda Yanga SC kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

Mchezaji huyo aliyefanya vizuri katika ligi kuu ya DR Congo sio mchezaji wa FC Lupopo, ni mchezaji wa Real Of Kinshasa alijiunga na FC Saint Eloi Lupopo kwa mkopo.

Klabu ya Yanga hadi sasa imetangaza usajili wa wachezaji watatu, KIUNGO Clatous Chama ambaye mkataba wake na Simba SC ulimalizika tangu June 30 mwaka 2024, na hawakutaka kumuongeza mkataba mpya, pamoja na Prince Dube ambaye amesajiliwa kama mchezaji huru akijivunjia mkataba na Azam FC. Hatimaye usiku wa kuamkia Julai 8 chuma kingine kikatambulishwa klabuni hapo.

Wanachokifanya Yanga kwa sasa ni kuwabakiza wachezaji wao tegemezi, na hadi sasa wamewaongeza mikataba wacheza kama Diarra, Mwamnyeto, Fardi Mussa, na Nickson Kibabage.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA NA KESI YA KUJIBU DHIDI YA KARIA....MANARA AIBUKA NA MAMBO YA SLOGAN...ATAKA SERIKALI IINGILIE KATI..