Home Habari za Yanga Leo RANGA CHIVAVIRO AKUBALI MZIKI WA YANGA…MSIKIE ALICHOSEMA

RANGA CHIVAVIRO AKUBALI MZIKI WA YANGA…MSIKIE ALICHOSEMA

Habari za Yanga- Ranga Chivaviro

Mshambuliaji  wa Kaizer Chiefs  Ranga Chivaviro ambaye aliwahi kuwindwa na Yanga akachomoa dakika za mwisho, alisema Yanga iliwaweka kwenye wakati mgumu ambapo nidhamu yao wakati hawana mpira ni ilikuwa  kitu kigumu kwao kuweza kuhimili.

Ranga Chivaviro ambaye ana asili ya Zimbabwe, alisema walikutana na kipimo kigumu katika mchezo wa kwanza wa kirafiki tangu waanze maandalizi.

“Ilikuwa ngumu kwetu, ni kama hawakutupa nafasi ya kujipanga wakati tukiwa tuna mpira, walikuwa wanalazimisha haraka tuupoteze uwe chini yao nadhani ndio silaha waliyoitumia kutengeneza ushindi kama ule,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Marumo Gallants.

“Unajua huu ulikuwa mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki wenzetu walionekana kuwa wepesi kuliko sisi ilitufanya kuonekana hatukuwa tayari kukutana na watu kama wao, nadhani tutabadilika kwa kuwa tupo chini ya makocha wapya ambao wanaaanza kutupa falsafa mpya.”

Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 4-0, ambapo walifanikiwa kutwaa taji la Toyota Cup, ikiwa ni kombe lao la  kwanza wa msimu wa 2024/25.

Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji wao mpya, Prince Dube,  na Kiungo Stephen Aziz  Ki, alifunga mabao 2 huku bao la nne likifungwa na Clement Mzize.

Ikiwa Afrika Kusini Yanga walicheza michezo mitatu, wameshinda miwili na kupoteza mmoja tena na timu ngumu kutoka Ujerumani FC Augsburg kwa mabao 2-1, bao  la Yanga lilifungwa na Jean Othos Baleke.

SOMA NA HII  WATANZANIA WAFELI MTIHANI WA UWAKALA FIFA...AFAULU MMOJA TU...