Home Habari za Yanga Leo NABI ATOA ANGALIZO KWA SIMBA…JIPANGENI VIZURI

NABI ATOA ANGALIZO KWA SIMBA…JIPANGENI VIZURI

Habari za Yanga SC

KOCHA Mkuu ambaye ametambulishwa hivi karibuni na Kaizer Chiefs, Nasredine Nabi amesema kuwa Yanga ina mabadiliko makubwa na chochote kinaweza kumkuta yoyote msimu ujao.

Nabi ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga, amekiri kwa uchungu kwamba kilichoomuumiza zaidi kwenye mechi ya juzi ni ukubwa wa kipigo ilichopata timu yake; “lakini tulistahili.”

Yanga tayari ipo nchini na kombe lao la Toyota walilobeba nchini Afrika Kusini ilipoweka Kambi ya muda ya maandalizi ikiichapa Kaizer Chiefs mabao 4-0.

Nabi ambaye hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza kubwa ya kirafiki baada ya kutoka kambini Morocco,alisema hata hivyo Yanga imebadilika na kuwapa shida ya kupoteza mpira kwa haraka wakati wanaumiliki iliyowalazimu wachezaji wake wengi vijana kushindwa kuhimili presha hiyo.

Aliongeza kuwa kitu ambacho imekutana nacho timu yake kinaweza kuikumba timu yoyote ndani na nje ya Tanzania msimu ujao ambayo haijajiandaa sawasawa kukutana na mbinu za namna hiyo za timu inayoweka presha kubwa kwa wapinzani wanapokuwa na mpira.

“Timu yetu ina wachezaji wadogo kidogo ambao hawakuwa tayari kukutana na ugumu wa namna ile, ukiangalia unaona namna ambavyo Yanga ilipokuwa haina mpira iliweka presha kubwa kwetu na vijana kujikuta wanafanya makosa makubwa,”alisema Nabi ambaye ambaye ana uraia wa Tunisia.

“Kuna mabao ambayo mliyaona ni kama yalikuwa zawadi kwao,lakini nadhani tumejifunza nadhani kilichotokea kwetu kinaweza kuikuta timu yoyote ambayo haikujiandaa sawasawa kukutana na mbinu za namna ile,”alisisitiza Kocha ambaye alikiri kwamba bado ana muda wa kuisuka timu yake.

SOMA NA HII  BAADA YA KUISAIDIA YANGA KUWA MABINGWA...DICKSON JOB AIBUKA NA HILI JIPYA TENA...ASISITIZA NI LAZIMA IWE HIVYO...