Home Habari za Yanga Leo WACHEZAJI 7 WA YANGA WALIOFANYA VIZURI AFRIKA KUSINI.

WACHEZAJI 7 WA YANGA WALIOFANYA VIZURI AFRIKA KUSINI.

HABARI ZA YANGA

Unaweza kusema Yanga sio inshu sana kupoteza mchezo wa jana,  kwani lengo sio ushindi ila lengo ni kutesti mitambo kuelekea Mashindano mbalimbali, katika mchezo dhidi ya FC Augsburg ambapo Yanga walipoteza kwa mabao 2-1, kuna baadhi ya wachezaji walionekana na kuonesha kiwango bora sana.

Uchambuzi wa wachezaji 7 wa Yanga walioonekana muda wote katika mechi  yao ya Kimataifa ya Kirafiki.

DAKIKA 64 ZA CHAMA

Kocha Gamondi alimuanzisha Chama na ndani ya muda huo, hakuonyesha kiwango kibovu wala kikubwa sana, akifanya yake kwa kutoa pasi za uhakika ambapo pasi yake moja ya mwisho nusura iipe Yanga bao katika dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza akimpa Maxi lakini shuti la Mkongomani huyo likagonga mlingoti wa lango.

BOKA, ABUYA NOMA

Beki wa kushoto Chadrack Boka naye alicheza mchezo huo akiingia kipindi cha pili kilipoanza akichukua nafasi ya mwenzake Nickson Kibabage.

Beki huyo alionyesha ubora wake wa kupandisha mashambulizi mbele pamoja na kurudi kwa haraka kukaba kwa haraka.

Mbali na Boka kiungo mzawa Aziz Andambwile naye alipewa muda kama huo akichukua nafasi ya Mudathir Yahya ambapo alionyesha kiwango kizuri akiziba vyema eneo la katikati kutopitika kirahisi na Wajerumani hao.

Kiungo mpya Mkenya Duke Abuya naye alipewa muda kama huo akionyesha ubora mkubwa wa kukimbiza mpira kwenda eneo la wapinzani sambamba na kutoa pasi zilizofika vizuri, huku shuti lake kali la dakika ya 54 lilikuwa ni shambulizi zuri kwa timu yake.

BALEKE NA BAO

Bao pekee la Yanga lilifungwa katika dakika ya 64 na mshambuliaji mpya Jean Baleke aliyeingia kipindi cha pili kumpokea Chama na kucheza mechi ya kwanza akiwa na uzi wa Yanga na akadhihirisha Wananchi hawakukosea kumsajili kwani alitumia dakika 22 tu uwanjani kufunga bao pekee la kufutia machozi.

Baleke alifunga bao hilo kwa kichwa kikali katika dakika ya 86 akiunganisha vyema krosi ya kiungo Nzengeli, japo dakika mbili nyuma alikosa umakini kumalizia pande jingine na Dube.

DUBE BAO LA WAZI

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Prince Dube aliyeingia kipindi cha pili alipata nafasi nzuri ya kufunga lakini shuti lake lilitoka nje kidogo ya lango.

DIARRA NA MAXI

Kipa wa Yanga,  Diarra aliyecheza mchezo mzima, alikuwa shujaa muhimu kwa timu yake akiokoa mashambulizi mengi ya hatari akidhihirisha kwamba timu yake haijakosea kumuongezea mkataba mwingine wa mwaka mmoja.

Mbali na Diarra, pia viungo Maxi, Stephanie Aziz KI walionyesha kwamba bado wako kwenye kiwango bora huku mabeki Yao Kouassi na Ibrahim Hamad ‘Bacca’ nao walikuwa imara kwenye ukuta.

SOMA NA HII  KISA AZIZ KI NA DIARRA....GAMONDI ASHUSHA PUMZI YANGA....MPANGO WAKE UKO HIVI...