Home Habari za michezo WAPINZANI WA SIMBA, YANGA NI HAWA…AZAM NA COASTAL PAGUMU

WAPINZANI WA SIMBA, YANGA NI HAWA…AZAM NA COASTAL PAGUMU

Habari za michezo, yanga na simba

Droo ya Mashindano ya Kimataifa Afrika, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la SHIRIKISHO zote zimechezeshwa Misri, na macho ya wengi yalikuwa ni kuwafahamu wapinzani wa Simba, Yanga, Azam FC, na Wagosi wa Kaya Coastal Union.

Yanga ambao watacheza Ligi ya Mabingwa wataanzia hatua ya awali ambap watakutana na timu ya Rwanda, Vital’O, baada ya kupita hapo atakutana na Commercial Bank ya Ethiopia au AS Villa ya Uganda.

Klabu ya Azam FC wao wataanza na APR FC ya RWANDA, akivuka hapo atakipiga na kina Fiston Mayele wa FC Pyramids katika hatua ya pili, ili kutinga hatua ya makundi.

Nafasi ya Yanga kwenda hatua y makundi huenda ikawa wazi kulingana na aina ya wapinzani aliopangiwa, lakini kwa upande wa Azam FC wao wana mlima mrefu wa kuupanda hadi kutinga hatua ya Makundi, kitu ambacho sio rahisi.

Kwa upande wa Mnyama SIMBA wao wataanzia hatua ya pili ambapo itasubiria mchezo wa kwanza Kati ya Uhamiaji FC ya Zanzibar dhidi ya Timu Bingwa FA toka Libya.

Mshindi wa mIchezo miwili ya mwanzo ambao wa Kwanza unachezwa Libya na wa Pili Zanzibar Ndio anaenda Kukutana na Simba kwa kuanzia Ugenini na kumalizia Uwanja wa Mkapa, na mshindi wa jumla Anaingia hatua ya Makundi kwa maana halisi Simba anaenda Makundi kwa ushindi wa michezo hiyo.

Klabu ya Coastal Union watakipiga na FC Bravos y Angola kisha endapo watapita, wataenda kukutana na FC Lupopo ya DR Congo.

MFUMO   WA UPANGAJI DROO UKOJE?

Kwa mujibu wa mfumo wa CAF kwenye klabu bingwa Afrika kupanga mechi za awali wana jumla ya makundi matatu, ambapo kuna timu tano ambazo hazitocheza hatua ya awali ( Preliminary) timu hizo ni Al Ahly, Esperance, Mamelodi, Petro na TP Mazembe.

Kisha kuna timu nne (4) ambazo zinatambuliwa kama HIGHEST RANKED yaani ziko na alama nyingi kwenye mfumo wa CAF ambazo timu hizo ni YANGA 🇹🇿, Pyramids, Raja na CR Belouzdad.

Kiufundi ukichukua hizo timu tano za juu kisha ukijumlisha na hizo nne basi unaenda kupata jibu ya timu bora Afrika kwa mujibu wa CAF kwenye klabu bingwa Afrika, Premier Club Competitions.

Lakini bado Yanga ataanzia hatua za awali sambamba na hao wenzake watatu, ni timu tano tu hazitoanzia hatua za awali.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali zipo 12 ambazo ni;

SIMBA SC- Tanzania
RS BERKANE- Morocco
FC LUPOPO- DR Congo
STADE MALIEN- Mali
ENYIMBA FC-Nigeria
ASEC MIMOSAS- Ivory Coast
ZAMALEK SC- Misri
USM Alger- Algeria
AS Vita- DR Congo
SHEKUKHUNE FC- Zambia
EL MASRY- Misri
CS Sfaxien- Tunisia

SOMA NA HII  MABOSI SIMBA WATUA NYUMBANI KWA KINA PACOME...MIPANGO YATEKELEZWA KIMYA KIMYA