Home Habari za Yanga Leo YANGA HAIFIKIRII USHINDI…USHINDANI WA NAMBA GAMONDI APAGAWA.

YANGA HAIFIKIRII USHINDI…USHINDANI WA NAMBA GAMONDI APAGAWA.

HABARI ZA YANGA-GAMONDI

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hawafikirii ushindi kwenye mechi za kirafiki hivyo kupata ushindi ni matokeo ambayo yanawaongezea nguvu kuendelea kupambana zaidi.

Ipo wazi kuwa Yanga imeweka kambi Afrika Kusini kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza Agosti 8 2024.

Julai 24 2024 Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TS Galaxy kwenye mchezo uliochezwa Afrika Kusini na bao pekee la ushindi lilifungwa na Prince Dube dakika ya 55 ikiwa ni bao lake la kwanza kwenye mechi za ushindani baada ya kutambulishwa kuwa mali ya timu hiyo.

Gamondi amesema: “Hatufikirii sana ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza hasa katika maandalizi ya msimu mpya kikubwa ni kuona kwamba kile ambacho tunajifunza kinafanyiwa kazi kwa umakini.”.

Mabingwa hao wa msimu wa 2023/24 wanatarajiwa kucheza mchezo wa Ngao wa Jamii Agosti 8 dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa.

USHINDANI WA NAMBA

Gamondi alieleza ushindani wa namba umeongeza kitu kikubwa kwa wachezaji na kuwafanya wawe na hari ya kupambana, kwani hakuna anaejiamini atapata nafasi kutokana na ubora wa kila mmoja wapo.

“Ninafurahia ushindani wa namba unavyoendelea kwenye kikosi changu kwani umewafanya wachezaji kujituma na kutafuta nafasi na hizo ni sifa za mchezaji anayecheza kwa malengo ambao ndio wapo sasa kwenye kikosi changu,” alisema kocha huyo raia wa Argentina.

SOMA NA HII  WAZAZI WALIOMPA MTOTO WAO MCHANGA JINA LA MAYELE WAFUNGUKA..."SIWEZI KUMBADILISHA JINA HATA IWEJE"...