Home Habari za Yanga Leo YANGA NA VITAL’O ZOTE KUPIGWA DAR…YANGA MTELEZO TU

YANGA NA VITAL’O ZOTE KUPIGWA DAR…YANGA MTELEZO TU

Habarii za Yanga leo

Klabu ya Vital’O ya Burundi imehamishia mechi yao ya nyumbani wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Chamazi Complex. Hii ni kutokana na Burundi kukosa uwanja ulioidhinishwa kwa ajili ya mechi za CAF.

Mabingwa wa hao wa Ligi Kuu bara msimu uliopita wamepangwa kuvaana na Vital’O FC ya Burundi kwenye mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Yanga itaanzia ugenini lakini itacheza mechi zote mbili ndani ya ardhi ya Tanzania.

Mchezo wa mkondo wa kwanza unatarajiwa kupigwa Agosti 16-18 katika dimba la Benjamin Mkapa huku mkondo wa pili ukipigwa Agosti 23-25 mwaka huu katika dimba la Azam Complex, Chamazi.

Ukaguzi uliofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) umebaini kuwa uwanja huo wa Intwali hauna sifa za kutumika kwa mashindano ya klabu Afrika kuanzia hatua ya awali.

Katika orodha ya viwanja iliyotolewa na CAF, hakuna jina la Uwanja wa Intwali jambo linalozilazimisha timu za Burundi zitakazoshiriki mashindano ya CAF msimu ujao kucheza mechi zao za nyumbani nje ya nchi yao.

Huo ni muendelezo wa timu za Burundi kucheza mechi za kimataifa za nyumbani nje ya nchi hiyo ambapo msimu uliopita zilitumia viwanja vya Azam Complex na Benjamin Mkapa vilivyopo Dar es Salaam.

Viwanja viwili vimepitishwa kutumika na timu za Tanzania ambavyo ni Benjamin Mkapa na Azam Complex.

Hiyo inamaanisha kuwa Uhamiaji na JKU za Zanzibar zitacheza mechi zao za nyumbani Dar es Salaam.

Msimu uliopita Yanga ilikutana na bahati kama hiyo kwenye mechi yake ya raundi ya kwanza ambapo timu ya El Merrikh ya Sudan ilitumia Uwanja wa Pele uliopo Kigali, Rwanda kutokana na Caf kutoupitisha Uwanja wa Omdurman wa kwao Sudan kutokana na sababu za kiusalama.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA SC AINDALIA MBINU MBADALA MARUNO GALLANTS KUELEKEA MECHI YA CAF